28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

China yampokea Mwanamfalme wa Saudia

BEIJING, CHINA

MWANAMFALME wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, amekuwa kwenye ziara ya kikazi nchini China ambayo licha ya utawala wa Saudia kuchafuliwa na kashfa ya mauaji ya mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi, lakini Serikali ya Beijing imeamua kulinda masilahi yake pamoja na kuongeza ushawishi wake kwenye taifa hilo.

Kiongozi huyo amekutana na makamu waziri mkuu wa China, Han Zheng, kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na kusaini mikataba mbalimbali ya kuimarisha biashara miongoni mwao.

Mazungumzo pamoja na makamu waziri mkuu, Han Zheng, yamefanyika kabla ya mwanamfalme huyo kuongoza warsha kuhusu ushirikiano kati ya nchi mbili.

Mikataba kadhaa imetiwa saini katika sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa wananchi mjini Beijing, kuhusu sekta ya mafuta, viwanda vya kemikali, uwekezaji, nishati mbadala na mapambano dhidi ya ugaidi.

Saudi Arabia ni mojawapo ya nchi zinazoipatia China mafuta ghafi na soko kuu pia kwa bidhaa zake ikiwa ni pamoja na ndege za kijeshi zinazoruka bila ya rubani. Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, jana mwanamfalme Mohammed bin Salman, alitarajiwa kukutana na rais wa China, Xi Jinping.

Jamhuri ya umma wa China ni kituo cha mwisho cha ziara ya mwanamfalme Salman iliyomfikisha pia Pakistan na India.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,186FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles