30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

CHINA YALIPA KISASI KWA MAREKANI

BEIJING, CHINA


MAMLAKA za CHINA zimeijibu Marekani kwa kuziongezea ushuru bidhaa zake kwa thamani ya Dola za Marekani bilioni 50.

Orodha ya bidhaa zilizolengwa na ushuru huo mkubwa ni pamoja na maharage ya soya, ndege, magari, mvinyo na bidhaa za kemikali.

Wizara ya Biashara na Wizara ya Fedha za China zimesema nyongeza ya asilimia 25 ya ushuru kwa bidhaa za Marekani inajumuisha bidhaa 106 zenye thamani ya kiasi hicho.

Tarehe ya kuanza kutekelezwa agizo hilo itategemea ni lini Marekani itaanza kutekeleza mpango wake.

Tangazo la China linakuja saa chache baada ya Marekani kuchapisha orodha ya bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 50, ambazo huenda zikatozwa ushuru.

Orodha hiyo ya Marekani inayojumuisha bidhaa 1,300 itapitiwa upya katika kipindi cha siku 60 zijazo kabla uamuzi wa mwisho kupitishwa, kuamua ni bidhaa zipi zitakazotozwa ushuru zaidi wa asilimia 25.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China, Lu Kang, ameyaeleza mapendekezo hayo ya Marekani kuwa hayana msingi na ni utaratibu wa kuyalinda masoko ya ndani.

“Hatua ya Marekani inapuuza manufaa yanayotokana na muundo wa ushirikiano wa kibiashara kati ya Marekani na China ambao umekuwepo kwa miongo minne iliyopita.

“Inapuuza miito ya jumuiya ya wafanyabiashara na masilahi ya watumiaji bidhaa katika nchi hizi mbili.

“Haina masilahi yoyote kwa uchumi wa China wala Marekani, na hata uchumi wa dunia,” alisema.

Tangazo hilo la China limesababisha mauzo makubwa ya hisa katika masoko ya kimataifa ya hisa na bidhaa nchini Marekani kuporomoka kwa asilimia 1.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles