23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

China yaishutumu Marekani

BERLIN, UJERUMANI

SERIKALI  ya China imeishutumu Marekani kwa kueneza hofu dhidi ya virusi vya corona badala ya kutoa msaada.

Kauli  hiyo  ya China inatokana na uamuzi wa Marekani kutangaza hali ya dharura na kupiga marufuku raia yeyote wa kigeni ambaye alitembelea nchini China kuanzia Desemba kutoingia nchini humo.

Si tu Marekani Hong Kong imefunga mpaka wake na China huku nchi kadhaa nyingine duniani nazo zikitangaza uamuzi kama huo.

Hadi sasa kesi za virusi hivyo  zilizothibitishwa ni zaidi ya 17,000 huku watu karibu 361 wakiwa wamekufa nchini China pekee.

Nje ya China kuna wagonjwa zaidi ya 150 waliothibitishwa kukumbwa na virusi hivyo na kifo kimoja kimetokea nchini Ufilipino.

Virusi hivyo vinasababisha mtu kushindwa kupumua sawasawa na kufanya maambukizi katika mfumo wa upumuaji na dalili zake huanza kwa homa kali  kikufuatia kifua kikavu.

HATUA ZA MAREKANI

Januari 23, Marekani iliamuru maofisa wake pamoja na familia zao kuondoka kwa dharura katika jiji la Wuhan  lililoko jimbo la Hubei ambako virusi hivyo vilianzia.

Siku chache kabla ya wiki, iliruhusu kuondoka kwa kujitolea kwa maofisa wake na waajiri wake wote walioko China.

Januari 30, Shirika la Afya duniani lilitangaza hali ya dharura kuhusiana na virusi hivyo.

Kutokana na hilo, Marekani iliamuru kuondoka kwa maofisa wake wote pamoja na familia zao wakiwamo wale wenye umri wa chini ya miaka 21.

Raia yeyote wa Marekani ambaye alikuwa Hubei akiingia nchini humo anawekwa karantini kwa siku 14.

UJERUMANI WAGONJWA WAFIKA 10

Wakati huo huo watu kumi wamethibitika kuugua ugonjwa wa virusi vya corona nchini Ujerumani.

Hatua hiyo imekuja baada ya watu wawili kati 124 waliosafirishwa kwa ndege ya Ujerumani kutoka mji wa China wa Wuhan ambao ni kitovu cha homa itokanayo na virusi vya Corona, kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo. 

Shirika la Msalaba Mwekundu lililotoa taarifa hiyo, limesema watu hao hivi sasa wamewekwa chini ya karantini katika hospitali ya mjini Frankfurt. 

Watu hao walithibitishwa kuwa na maambukizi wakati vipimo vilipochukuliwa katika kambi ya jeshi ya Germasheim, ambako watu waliotoka Wuhan wamepewa hifadhi. 

Waziri wa afya wa Ujerumani, Jens Spahn amesema amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Marekani, na wamekubaliana juu ya haja ya mawaziri wa jumuiya ya nchi saba zilizoendelea kiviwanda, G7 kukutana kupanga mkakati wa pamoja dhidi ya homa hiyo hatari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles