27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

China yafanya majaribio ya kijeshi Taiwan

 BEIJING, CHINA 

CHINA imetangaza kutekeleza jaribio la kijeshi karibu na njia ya bahari ya Taiwan wakati mjumbe mwandamizi wa Marekani akifanya ziara katika mji mkuu wa Taipei na kuonekana kupuuza vitisho vya Beijing.

Msemaji wa jeshi la China PLA, kanali Zhang Chunhui amesema mazoezi hayo ya kijeshi ni muhimu kwa kukabiliana na hali ya sasa katika njia ya bahari ya Taiwan na kwamba yatasaidia katika ulinzi wa kitaifa.

China inadai kuwa Taiwan ambayo inajitawala yenyewe, ni moja ya mikoa yake na inazikataza nchi nyingine kuwa na uhusiano nayo rasmi.

Hata hivyo, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Keith Krach aliwasili Taiwan Alhamisi kuhudhuria ibada ya kumbukumbu ya rais wa zamani Lee Teng-hui.

Ziara ya Krach ni ya pili kufanywa na ofisa wa juu wa Marekani katika muda wa miezi miwili baada waziri wa afya, Alex Azar kuwa ofisa wa kwanza wa ngazi ya juu wa Marekani kufanya ziara Taiwan tangu mwaka 1979.

Wakati huo huo Mpaka wa Belarus na Poland umesalia kuwa wazi licha ya Lukashenko kuagiza kufunga mipaka yake.

Walinzi wa mpaka wa Poland wamesema mpaka kati ya Belarus na Poland umesalia wazi Ijumaa asubuhi baada ya Rais wa Belarus Alexander Lukashenko kusema nchi yake inahitaji kufunga mipaka yake na Poland na Lithuania.

Ofisa mmoja wa Poland ambaye amekataa kutambuliwa kwa sababu hana ruhusa ya kuzungumza na waandishi habari amesema mpaka huo uko wazi na hakuna ishara kuwa utafungwa

Lukashenko ambaye anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu baada ya wiki kadhaa za maandamano, alisema jana Alhamisi kuwa Belarus inahitaji kufunga mpaka wake na Poland na Lithuania na kuimarisha doria katika mpaka wake na Ukraine.

Belarus imetumbukia katika mzozo wa kisiasa kufuatia uchaguzi mkuu wa Agosti 9 uliogubikwa na madai ya wizi wa kura na kusababisha maandamano makubwa dhidi ya Lukashenko ambaye amekuwa madarakani tangu 1994.

Lukashenko anasema alishinda uchaguzi huo kwa njia ya haki na kuwa yeye ni mhanga wa kampeni chafu inayoendeshwa na mataifa ya Magharibi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles