30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

China kuzindua mwezi bandia 2020

JOSEPH HIZA NA MTANDAO

CHINA imepanga kuzindua mwezi wake bandia ifikapo mwaka 2020, ambao utachukua nafasi ya taa za mitaani na hivyo kupunguza gharama za umeme katika maeneo ya mijini.

Kwa maneno mengine kazi kuu ya mwezi huo wa kutengenezwa na binadamu utakuwa ni kuangazia miji nyakati za usiku badala ya taa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa, taasisi moja binafsi ya masuala ya anga za juu iliyoko mjini Chengdu inataka kuzindua ‘kituo cha satelaiti’ kitakachoangaza ulimwengu.

Kwa kuakisi mwanga kutokea jua, satelaiti hiyo itakayochukua taa za mitaani katika maeneo mijini, itaokoa kiasi kinachokadiriwa kufikia dola milioni 170 za Marekani zikiwa gharama za umeme kwa jiji la Chengdu, iwapo miezi ya kutengenezwa na mwanadamu itaangazia eneo la kilomita mraba 50.

Aidha chanzo cha mwanga kutoka jua pia kitasaidia juhudi za uokozi katika kanda zinazokabiliwa na majanga wakati wa mkatiko wa umeme.

Mpango huo umevutia hisia mbalimbali kutoka kwa wanasayansi ambao wanahoji uwezekeno wa kufanikiwa huku wengine wakiukejeli.

Hakuna mengi yaliyoangaziwa kuhusiana na mradi wenyewe – taarifa zilizotolewa kwa umma pia zinaonekana kukinzana.

Gazeti la Taifa la People’s Daily la China liliangazia mradi huo kwa mara ya kwanza miezi miwili iliyopita.

Gazeti hilo lilimnukuu mwenyekiti wa Taasisi ya Masuala ya Anga za juu ya China, Wu Chunfeng aliyegusia mpango huo.

Wu amesema mradi huo mpya umekua ukifanyiwa majaribio kwa miaka kadhaa sasa na kwamba teknolojia hiyo iko tayarikuzinduliwa ifikapo mwaka 2020 katika Kituo cha Kuzindulia Satelaiti cha Xichang huko Sichuan.

Alisema kwamba iwapo majaribio ya mwezi huo yataenda vyema, miezi mingine mitatuitafuata mwaka 2022.

Mkuu huyo wa Chama cha Sayansi ya Eneo Jipya Tian, kinachohusika na mradi huo, hatahivyo hakubainisha iwapo mpango huo umeidhinishwa rasmi na serikali.

Mwezi bandia utafanyaje kazi?

Kwa mujibu wa People’s Daily, mwezi huo utafanya kazi kama kioo, ambacho kitakuwa kikielekeza mwangaza wa jua duniani

Utakuwa unazunguka karibu kilomita 500- sawa na urefu wa kituo cha kimataifa cha anga za juu.

Mzunguko wa mwezi duniani unakadirika kuwa kilomita 380,000.

Ripoti hiyo haijatoa maelezo yoyote kuhusu muonekano wa mwezi huo bandia.

Lakini Wu amesema utakua ukileta mwangaza wa jua katika eneo kilomita 10 na kilomita 80 na utakua na unaangaza mara nane zaidi ya mwezi wa ukweli.

Wu anasema mwangaza wa mwezi huo bandia utadhibitiwa ili kupunguza gharama.

Pia anasema mwangaza wa mwezi bandia wanaamini utakuwa wa gharama nafuu kuliko gharama zinazotokana na matumizi ya taaza barabarani au mitaani.

Dk. Matteo Ceriotti, mhadhiri wa somo la uhandisi wa anga za juu katika Chuo Kikuu cha Glasgow nchini Uingereza, amesema “Nadhani huu ni mfano wa uwekezaji wa aina yake,”

“Umeme unaotumika usiku nighali mno kwa hivyo kukipatikana mwangaza mbadala kwa miaka 15 utachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uchumi.”

Lakini hilo linawezekana?

Kisayansi kuna uwezekano asema Dr Ceriotti.

Hata hivyo ili kufikia lengo lake, mwezihuo bandia lazima uwe unazunguka eneo la Chengdu – katika eneo ambalo ni dogo ukilinganisha na mduara wa dunia kutoka angani.

Mradi huu utakua na athari gani kwa mazingira?

Watumiaji wa mitandao wa kijamii nchini China, baadhi yao wanasema tayari kuna uchafuzi wa mazingira unaotokana na mwangaza katika eneo la Chengdu na miji mingine ya China.

Wengine wanasema mwangaza huo bandia utakua na athari kwa viumbe wengine wadogo duniani.

John Barentine, mkurugenzi wa Sera ya Umma katika Chama cha Kimataifa cha Anga za Juu ameukosoa mradi huo.

Aliliambia Jarida la habari la Forbes kuwa mwezi huo utaongeza mwangaza wakati wa usiku katika jiji ambalo tayari linakabiliwa na mwanga mkali wa jua, na hivyo hakuna haja ya kuwaongezea matatizo zaidi wakazi wa Chengdu,

Dk. Ceriotti pia amesema endapo mwangaza utakua mkali zaidi huenda ukaathiri mfumo wa usiku wa maumbile yadunia hali ambayo pia huenda ikawa na athari kwa wanyama.

Pia amesema ikiwa mwangaza huo utakua mdogo hautakuwa na maana yoyote.

Wakati program za anga za juu za Cghina zikiwa katika ushindani wa kuzifikia zile za Marekani na Urusi, idadi kadhaa ya miradi yaaina yake iko njiani ikiwamo mwezi wa uchunguzi ujulikanao kama Chang’e-4.

Mradi huo umepangwa kuzinduliwa baadaye mwezi huu na iwapo utafanikiwa, utakuwa wa kwanza kuchunguza ‘upande wa giza’ wa mwezi.

China si taifa la kwanza kujaribu kuakisi mwanga wajua kwa dunia kwani katika miaka ya 1990, wanasayansi wa Urusi waliripotiwa kutumia vioo kikubwa kuakisi mwanga kutoka anga za juu katika mradi wamajaribio ufahamikao kama Znamya au Banner.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles