27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CHINA KUTOA BILIONI 60/- NCHI ZA AFRIKA

KONGAMANO: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa kongamano la biashara kati ya Tanzania na China jijini Beijing nchini China juzi. Picha: Ofisi ya Waziri Mkuu

Na MWANDISHI MAALUMU-CHINA             |            


RAIS wa China, Xi Jinping amesema nchi yake  itatoa  dola za Marekani bilioni 60   kwenye mpango wake wa miaka mitatu ya ushirikiano na Afrika katika maendeleo.

Ameyasema hayo jana  wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC),   Beijing,  China.

Rais Jinping ameahidi kuwa nchi yake itatoa ushirikiano  kuhakikisha   amani ya kudumu inapatikana barani Afrika, hatua ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.

Maeneo mengine ambayo Rais huyo ameahidi   China kulisaidia Bara la Afrika ni   ujenzi wa miundombinu na ushirikiano katika sekta ya biashara  na huduma za afya.

Alisema nchi yake itatoa nafasi za mafunzo ya kilimo bora na mafunzo ya ufundi kwa watalaamu kutoka Afrika ili kuchangia katika maendeleo ya uchumi.

Alisema hivi sasa anaamini China na nchi za Afrika ziko karibu zaidi na zinashirikiana vizuri   katika shughuli za maendeleo ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye anamuwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika mkutano huo alisalimiana na Rais Jinping baada ya ufunguzi.

Mkutano huo utaendelea leo ambako viongozi wengi kutoka   Afrika watapata fursa ya kuzungumza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles