27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

China kujenga kambi nne kijeshi Afrika

BEIJING, CHINA

CHINA inafikiria kujenga kambi za kijeshi katika nchi nne za Afrika kwa mujibu wa ripoti ya idara ya ulinzi ya Marekani.

Mpango huo, umebainishwa kupitia ripoti iliyochapishwa wiki iliyopita nchini humo na kuangaziwa na vyombo vya habari, huku baadhi ya nchi ambazo kambi hizo zitajengwa zikikanusha kufanya mazungumzo na China.

Nchi hizo zinazotarajiwa kunufaika na mpango huo, ni pamoja na Tanzania, Kenya, Shelisheli na Angola, zimetajwa kuwa miongoni mwa nchi kadhaa ambazo inapania kujenga kambi za kijeshi.

Wakati China ikibainisha hayo, Serikali za nchi hizo zilizotajwa na Marekani hazijatoa tamko lolote kuhusiana na suala hilo.

“Kando na kambi yake ya sasa nchini Djibouti, Jamhuri ya watu wa China ina mpango wa kuongeza kambi zake za kijeshi ughaibuni kusaidia vikosi vya majini, angani na ardhini.” Imeeleza sehemu ya ripoti 

China imeamua sehemu itakapojenga vituo vyake vya kijeshi nchini Myanmar, Thailand, Singapore, Indonesia, Pakistan, Sri Lanka, Umoja wa Falme za Kiarabu,(UAE), Kenya, Ushelisheli, Tanzania, Angola, na Tajikistan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles