20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

CHERCHESOV: TULIKOSA WACHEZAJI BORA

SOCHI, URUSI


BAADA ya Urusi kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini humo, kocha wa timu hiyo, Stanislav Cherchesov, ameweka wazi kuwa walikosa wachezaji bora lakini walikuwa na timu bora.

Urusi ambao walikuwa wenyeji wa michuano hiyo, wametolewa katika hatua ya robo fainali dhidi ya Croatia kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3, baada ya sare ya 2-2 katika dakika 120.

Kocha wa Urusi, Cherchesov, amesema hakuwa na wachezaji bora wanaounda kikosi chake, lakini walikuwa na wachezaji ambao waliweza kutengeneza timu na kuwafanya wafikie hatua hiyo.

Waliweza kuingia hatua hiyo ya robo fainali baada ya kuwaondoa mabingwa wa michuano hiyo mwaka 2010, Hispania kwa mikwaju ya penalti lakini wameshindwa kufanya hivyo mbele ya Croatia.

“Ni aibu kwa kuwa tumetolewa, lakini nadhani tumestahili kufika hapa, tulicheza vizuri michezo yetu tukiwa na wachezaji wazuri, kwa hali ya kawaida tunaweza kusema tulicheza kama tulivyopanga, ila tumeshindwa kufikia malengo yetu hivyo ndivyo soka lilivyo.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wachezaji wote, mashabiki kwa sapoti yao na kutufanya tuwe hapa, kuna makosa tuliyafanya na ndio maana tumeshindwa kuendelea na wenzetu waliweza kutumia makosa yetu.

“Ukweli ni kwamba kwenye Kombe la Dunia hatukuwa na wachezaji bora, lakini tulikuwa na timu ya wachezaji 23 ambao walionesha kupambana tangu siku ya kwanza hadi tunatolewa, tunashukuru sana,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles