28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Chanzo cha mtindio wa ubongo, mimba kuharibika chaelezwa

NA SAMWEL MWANGA
SERIKALI imesema watoto wanaozaliwa na mtindio wa ubongo na kuharibika mimba kwa  kina mama ni miongoni mwa athari zinazotokana na  kukosekana matumizi ya chumvi yenye madini joto.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mratibu wa Lishe Mkoa wa Simiyu, Dk. Chacha Magige  alipotembelea mgodi wa chumvi uliopo katika kijiji cha Nyalanja wilayani humo   kufahamu   athari zinazotokana na matumizi ya chumvi isiyo na madini joto.

Dk. Magige alisema   ni lazima kwa wachimbaji  hao wa chumvi kuboresha biashara ya chumvi kwa kuongeza madini joto  kukuza soko  na kuwaepusha watumiaji na madhara ya kiafya.

Alisema  wamekuwa wakifanya ziara ya mara kwa mara katika mgodi huo na kukutana na wachimbaji hao na kila mara huwakumbusha madhara ya kutumia  chumvi isiyo na madini joto  kwa sababu  kuna madhara zaidi ya  104 yanayosababishwa   na ukosefu wa madini hayo.

 “Athari zinazotokana na kutotumia chumvi yenye madini joto ziko nyingi mojawapo ndiyo hiyo kwamba tunapata watoto ambao wana mtindio wa ubongo, watoto hawakui vizuri ule udumavu wa watoto lakini pia kuna kuharibika kwa mimba kwa kinamama wajawazito,”alisema.

Aliwataka wazalishaji wa chumvi kuhakikisha wanaweka madini joto  kuepuka kuwasababishia walaji madhara kwa vile  madini hayo hutolewa bure bila gharama yoyote pamoja na wananchi kuitumia vizuri elimu ya matumizi ya chumvi hiyo ambayo hutolewa kupitia njia mbalimbali.

Dk. Magige alisema mikakati ya mkoa huo kuwakomboa wakazi wa wilaya  ya Meatu maeneo mengine ya nchi  kutoka katika matumizi ya chumvi isiyo na madini joto ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanahabari  waweze kujua ukubwa wa tatizo na kupanga mikakati ya kuweza kuisaidia jamii.

“Lakini mkakati mwingine ambao tumejiwekea kama mkoa ni kuipeleka hii elimu pia kwa watu wa afya ngazi ya jamii tunaita ‘community health workers’.

“Hawa pia wameandaliwa  mafunzo yao ambayo ni  tofauti kidogo, wao wataenda kufundishwa ukubwa wa tatizo lakini pia kuwatengenezea mkakati wa namna gani watashirikiana na jamii kuhakikisha kwamba chumvi inakuwa na madini joto,” alisema.

 Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dk. Joseph Chilongani alisema  wilaya hiyo imechukua hatua ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya chumvi isiyo na madinijoto na wengi wao kwa sasa hawaitumii chumvi isiyo na madini joto inayopatikana katika kijiji cha Nyalanja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles