30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI CHATAJWA

Na RAMADHAN HASSAN-CHAMWINO                |                  


IMEELEZWA kuwa changamoto ya wazazi kupenda mahari na kuwaoza watoto wao wakiwa wadogo, ni miongoni mwa sababu zinazochangia ukatili wa jinsia na mimba za utotoni kuzidi kuongezeka wilayani Chamwino.

Hayo yalielezwa juzi na baadhi ya viongozi wa vikundi mbalimbali vya kuelimisha rika kupitia mradi unaosimamiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la WOWAP, kwa  ufadhili wa The Foundation for Civil Soceity ukiwa na  lengo la kutokomeza ukatili wa  jinsia na mimba za utotoni.

Mmoja wa viongozi hao, Nyamwanji Nyamwanji, alisema ingawa Serikali imesema elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, lakini jamii bado haioni umuhimu wa elimu na kukimbilia kuwaoza watoto.

Alisema tatizo lililopo hivi sasa wazazi wengi hawaoni umuhimu wa elimu jambo ambalo linasababisha wanafunzi wa kike   wasione umuhimu.

“Kwa kweli changamoto ya jambo hili tunalopambana nalo bado ni kubwa kwa sababu wazazi wengi wanathamini mahari kuliko elimu ya watoto wao wa kike.

“Tunaiomba Serikali nayo iliangalie jambo hili kwa vile  watoto wengi wanakatisha masomo yao,” alisema.

Alisema wao kama viongozi wa vikundi wamebaini lipo tatizo la wazazi wengi kutowajibika kwa watoto wao katika matumizi jambo ambalo nalo linachangia kujiingiza katika mambo yasiyofaa na vishawishi.

“Suala la rushwa nalo ni kikwazo kwa sababu  sheria ingefuatwa na baadhi ya watu wanaowaoa watoto au kuwapa mimba wangehukumiwa kwenda jela, ingeweza kuwa funzo kwa wengine na kuacha kuwachezea watoto hao wadogo,” alisema.

Naye Mratibu wa Mradi huo kutoka WOWAP, Nasra Suleimani, alisema wanaendelea kuwafuatilia viongozi hao katika kuwakumbusha majukumu yao ya kutoa elimu kwa jamii  jambo hilo liweze kutokomezwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles