30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Chanjo ya malaria kwa watoto yafanyiwa majaribio Malawi

LILONGWE, MALAWI

CHANJO ya kwanza ya malaria duniani inayofahamika kama RTS,S imeanza kufanyiwa majaribio nchini hapa.

RTS,S ina mchanganyiko wa dawa inayosaidia mfumo wa kinga mwilini kukabiliana na mbu wanaosababisha malaria.

Majaribio ya awali ya chanjo hiyo yalionesha kuwa inafanya kazi kwa asilimia 40 kwa watoto wa kati ya miezi mitano hadi saba.

Visa vya ugonjwa wa malaria vimeongezeka tena baada ya miongo kadhaa ya kukabiliana nao.

Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, visa vya ugonjwa huo duniani vinaendelea kuongezeka, hali ambayo imezua hofu huenda ikarudisha nyuma juhudi zilizopigwa kukabiliana nao.

Zaidi ya asilimia 90 ya watu 435,000 waliopata maradhi ya malaria barani Afrika walifariki dunia huku watoto wakiathiriwa zaidi.

Malawi ambayo iliripoti karibu visa milioni tano vya ugonjwa wa malaria mwaka 2017, imechaguliwa kufanyiwa majaribio ya chanjo hiyo.

Mataifa mengine yatakayofanyiwa majaribio ya chanjo hiyo ni Kenya na Ghana, yakiwa yamechaguliwa kwa sababu tayari yanaendesha kampeni kubwa ya kukabiliana na ugonjwa huo, huku visa bado vikiwa juu.

Chanjo hii imekuwa ikifanyiwa utafiti kwa zaidi ya miaka 30, ikichangiwa kiasi kinachokadiriwa kuwa dola bilioni moja na mashirika kadhaa.

Majaribio ya chanjo hiyo yanaongozwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ambalo linasema hii ni mara ya kwanza kinga ya malaria kutolewa kwa watoto.

Mbali ya chanjo hii mpya kuelezwa kufanya kazi kwa asilimia 40 ikilinganishwa na chanjo nyingine, huimarisha kinga zaidi kwa sababu vyandarua vya kuzuia mbu na dawa nyingine tayari zinatumika.

“Chanjo hii ina uwezo wa kutoa kinga kwa asilimia 90 au zaidi, kwa maoni yangu si kitu tunachokiangazia kwa sasa,” kituo cha Bloomberg kilimnukuu ofisa wa WHO, Mary Hamel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles