27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Chanjo ya Ebola yafanyiwa tathmini Afrika Mashariki

NEW YORK, Marekani

WAKATI  timu za wanaokabiliana na ugonjwa wa  Ebola wakihangaika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanasema wanatambua hatari zake na wanatathmini kuanza kutumia chanjo ya Ebola iliyoko katika majaribio.

Katika kipindi cha hivi karibuni, vituo vinavyo tibu Ebola nchini  DRC vimekuwa vikishambuliwa na waasi  hivyo wafanyakazi wanaokabiliana na ugonjwa huo wameshindwa kufikia maeneo yenye milipuko.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswali ya Marekani (VOA), vyanzo vya habari Afrika Mashariki vimeripoti kuwa hivi sasa nchi sita, hasa zile zilizoko mpakani na majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri nchini DRC, ambako milipuko ya ugonjwa huo iliendelea kwa kasi, wanakabiliana na vikwazo vyote kuhakikisha wanaweza kwa ufanisi kufikisha matibabu pale ambapo imethibitishwa Ebola ipo.

VOA ilieleza kuwa Uganda, Burundi na Rwanda ni maeneo yaliyo na hatari kubwa ya maambukizi, wakati baadhi ya sehemu za Sudan Kusini na Tanzania ambayo yako karibu na miji iliyoko mpakani yanakabiliwa na hatari ya wastani ya maambukizo hayo.

Gazeti la The East African limemnuku Kaimu Mkuu wa Idara ya Afya kwenye Sekretarieti ya EAC Arusha, Dk. Michael Katende, akieleza uamuzi wa kutumia chanjo ya Ebola, akisema kwamba  ni jambo la busara kuwakinga wafanyakazi walioko mstari wa mbele kukabiliana na ugonjwa huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles