22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

CHAMBUA AMLILIA CHAMANGWANA


NA SAADA SALIM   |

KOCHA wa zamani wa Yanga Mmalawi, Jach Chamangwana, amefariki dunia akiwa na miaka 61 baada ya kusumbuliwa na maradhi.

Chamangwana alifariki juzi katika Hospitali ya Malkia Elizabeth iliyopo mji wa Blantyre nchini Malawi alikokuwa amelazwa.

Akizungumza na MTANZANIA, mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, ambaye aliwahi kufanya kazi na Chamangwana akiwa mchezaji na kocha msaidizi, alisema kifo cha kocha huyo ni pigo kwa wapenzi wa soka Tanzania kutokana na mchango alioutoa.

“Hizi taarifa nimezipokea kwa masikitiko makubwa, nimefanya naye kazi mara mbili, nikiwa mchezaji na baadaye aliniandaa kwa ajili ya kuwa msaidizi wake, nilifanikiwa kupata elimu ya ukocha na kufanya naye kazi kwa muda mrefu.

“Alinifundisha kanuni na sheria za ualimu wa mpira wa miguu, hakika nitamkumbuka daima,” alisema Chambua.

Chambua aliendelea kusema kuwa Chamangwana alikuwa kocha mwenye uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo, kisha kutumia mbinu zilizomwezesha kupata ushindi.

“Sikuwa na fikra za kuwa kocha, lakini kwa kuwa alinielewa vizuri na jinsi nilivyokuwa nawasiliana na wachezaji wenzangu, alinishauri nisome ukocha.

“Hii leo (juzi) napata taarifa za kusikitisha kwamba hatuko naye tena, hakika ni kocha wa kukumbukwa kutokana na elimu aliyoniachia,” alisema Chambua.

Akiwa na Yanga, Chamangwana, aliiwezesha kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mbali ya kuwa kocha, Chamangwana aliwahi kukipiga katika klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini akicheza nafasi ya ulinzi, alipewa jina la ‘Black Stone’ likiwa na maana mwamba mweusi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuwakabili washambuliaji wa timu pinzani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles