23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CHAMBERLAIN: SIOMBI RADHI KUONDOKA ARSENAL

LONDON, ENGLAND

KIUNGO mpya wa klabu ya Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain, amedai maamuzi yake ya kuondoka katika klabu ya Arsenal na kujiunga na kikosi cha kocha Jurgen Klopp, yalikuwa magumu kwake, lakini hawezi kuwaomba radhi mashabiki kuondoka kwake.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na kikosi cha Arsenal tangu mwaka 2011, kabla ya kujiunga na Liverpool katika kipindi hiki cha majira ya joto dakika chache kabla ya kufungwa kwa usajili.

Mchezaji huyo amejiunga na Liverpool kwa kitita cha pauni milioni 35, baada ya kukataa ofa kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, Chelsea, lakini amedai Arsenal ni sehemu ya maisha yake, hivyo kufanya maamuzi ya kuondoka, jambo ambalo lilikuwa gumu kwake.

Katika kipindi cha miaka sita aliyokaa ndani ya kikosi hicho cha Arsenal alifanikiwa kushinda taji la Kombe la FA mara tatu.

“Kuondoka Arsenal yalikuwa maamuzi magumu sana katika maisha yangu, kwanza napenda niwashukuru mashabiki wa klabu hiyo ya Arsenal kwa sapoti yao waliyonipa katika kipindi changu chote, lakini siwezi kuomba radhi maamuzi yangu ya kuondoka.

“Niliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kufungua ukurasa wangu mpya wa maisha ya soka, sikutaka kuondoka huku nikiwa na mgogoro na timu, nadhani ulikuwa wakati wangu sahihi wa kufanya hivyo.

“Wakati nipo Arsenal nilikuwa namwangalia kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp kila anachokifanya kwa wachezaji wake, hivyo nilivutiwa kwa kiasi kikubwa na nilitamani kuwa mmoja wa wachezaji wake.

“Klopp ni mmoja wa makocha ambao wanaweza kukushawishi, kukujenga, hivyo nikaona bora niondoke Arsenal ili niyapate hayo kwa Klopp, ninaamini hapa nilipo nitafanikiwa kwa hilo, kutokana na uwezo wa kocha pamoja na umoja wa wachezaji, kutokana na hali hiyo naweza kuja kuwa mmoja wa wachezaji wenye uwezo mkubwa duniani,” alisema Chamberlain.

Mchezaji huyo katika klabu ya Arsenal alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 132 ya Ligi Kuu tangu ajiunge mwaka 2011 na kufanikiwa kufunga mabao tisa, wakati huo kabla ya kujiunga na Arsenal alikuwa anakipiga katika kikosi cha Southampton, huko alicheza michezo 36 ya Ligi na kufunga mabao tisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles