30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

CHAMBERLAIN AJIUNGA RASMI LIVERPOOL

LONDON, ENGLAND

HATIMAYE klabu ya Liverpool, imekamilisha uhamisho wa kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, kwa mkataba wa miaka mitano.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, amekamilisha uhamisho wake kwa kitita cha pauni milioni 35 na kuwekewa mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki chini ya kocha Jurgen Klopp.

Uhamisho wa mchezaji huyo umekamilika ikiwa mchezaji huyo yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England kujiandaa na michezo ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Hata hivyo, kulikuwa na mvutano kati ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea ambao walionesha nia ya kutaka kumsajili kabla ya kufungwa kwa dirisha usiku wa kuamkia leo, lakini Liverpool wakafanikiwa kukamilisha uhamisho huo.

Siku moja kabla ya kukamilika kwa usajili wake, mchezaji huyo aliweka wazi kuwa hawezi kujiunga na Chelsea kwa kuwa anaamini hawezi kupata nafasi ya kucheza kama kiungo wakati Chelsea wakitaka kumtumia kama mshambuliaji wa pembeni.

Klabu ya Arsenal ilikuwa na mipango ya kutaka kuendelea kuwa na mchezaji huyo kwa kipindi kirefu huku kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger, akimwekea ofa ya pauni 180,000 kwa wiki, lakini Chamberlain alikataa kubaki na kuamua kukubali pauni 120,000 kwa wiki ndani ya Liverpool.

Kupitia mtandao wa klabu ya Liverpool, waliweka picha ya mchezaji huyo akiwa amevaa jezi yao mara baada ya kukamilisha uhamisho wake.

“Karibu sana Chamberlain katika klabu ya Liverpool, tunatarajia makubwa kutoka kwa mchezaji huyo katika kipindi hiki cha michuano mbalimbali,” waliandika.

Hata hivyo, mchezaji mwenyewe ameonekana kuwa na furaha kubwa kukamilisha uhamisho huo ikiwa alibakiwa na mwaka mmoja wa kumaliza mkataba wake ndani ya Arsenal.

“Ninaamini ndoto zangu zimekamilika, Liverpool ni miongoni mwa klabu kubwa barani Ulaya, hivyo kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho ni jambo la kujivunia kwa upande wangu, lengo langu kubwa siku moja kuja kuwa kama Steven Gerrard,” alisema Chamberlain.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles