26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Chama cha Wafugaji Tanzania chawasaidia wafugaji waliochomewa maboma

JANETH MUSHI-BABATI

Chama cha Wafugaji Tanzania, kimetoa msaada wa maturubai kwa kaya zaidi  30 zilizoteketezwa kwa moto  katika kijiji cha Vilimavitatu wilayani Babati, kwa ajili ya kujisitiri na baridi nyakati za usiku pamoja na jua kali nyakati za mchana.

Zaidi ya maboma 30 kijijini hapo yanayokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 300 yalichomwa mwanzoni mwa wiki iliyopita na kusababisha familia hizo kukosa mahali pa kuishi, wakidaiwa kujenga eneo la shoroba za wanyama katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori(WMA) ya Burunge.

Msaada huo umetolewa leo Jumamosi Julai 13,  na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, George Bajuta, katika eneo la jangwani, katika kata ya Nkaiti, ambapo amesema baada ya kujionea mazingira magumu wanayoishi wananchi hao ikiwemo kulala chini ya miti wamelazimika kutoa misaada hiyo ili kuweza kuwanusuru na baridi hasa watoto.

“Tumeamua kuwakabidhi misaada hii ili walau mjisitiri na kujiokoa na baridi, sisi kama chama kazi yetu ni kulinda na kutetea haki na maslahi ya wafugaji na tutaendelea kushirikiana na nyie mpaka mpate haki zenu,”amesema.

Mmoja wa wananchi hao Dorcas Payai alishukuru kwa msaada huo ambapo amesema wanawake na watoto wamekuwa wakiteseka hasa ikizingatiwa baridi kali ambayo ipo katika eneo hilo ambapo leo ni siku ya sita hawana mahali pa kulala kufuatia kuchomwa kwa maboma yao.

Kwa upande wake Mratibu wa Migogoro na malisho kutoka chama hicho, Jeremiah Wambura,amesema migogoro katika maeneo ya wafugaji inapaswa kukomeshwa ili kuwawekea wafugaji mazingira rafiki ya kufanya shughuli zao na kuwataka wananchi hao kuwa watulivu wakati suala hili linashughulikiwa.

“Tunaamini Rais Dk.Magufuli ni kiongozi wa wanyonge na kilichotelekezwa hapa siyo mpango wa Rais, niwaombe ninyi siyo wanyonge kwenye nchi yenu kuweni watulivu naamini adha hii itakoma haitowarudia tena,tumeamua kujitoa  kwa ajili yenu kwani maeneo mengi wafugaji  wanapata tabu na tutashirikiana kumaliza tatizo hili”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles