23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Chama awarusha roho Yanga

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama, ameendelea kuwarusha roho wapenzi wa timu ya Yanga SC, akidhihirisha kuwa hawezi kuondoka kirahisi baada ya kusema ‘Simba ndio baba lao.’

Hivi karibuni ziliibuka tetesi kuwa Chama, ameingia katika rada za Yanga na wanatarajia kumsajili, uvumi uliochangiwa na Makamu Mwenyekiti wa Wanajangwani hao Fredrick Mwakalebela.

Chama ametumia mtandao wake wa Instagram, akiisifia timu yake, akitumia kibwagizo cha wimbo wa mwanamuziki, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’ akisema ‘Simba Baba Lao’.

Kiungo huyo raia wa Zambia alijizolea umaarufu hapa nchini kutokana na kiwango chake, amekuwa katika presha ya mashabiki wanaohofia kuwa anaweza kuondoka.

Katika video hiyo, pamoja na kuisifia Simba, Chama alitaja mabao yake bora aliyoifungia timu hiyo tangu aliposajiliwa mwaka 2018.

Bao la kwanza aliloifunga timu ya Sevilla inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania, mchezo huo ulikuwa wa kirafiki huku Simba wakifungwa mabao 5-4, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Lingine ni lile aliloifunga AS Vita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Simba ilipopata ushindi wa 2-1, Uwanja wa Taifa na kutinga robo fainali.

Bao lake bora namba tatu ni dhidi ya Nkana FC katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba iliposhinda mabao 3-1.

“Kwa upande wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, nimefunga mabao mengi mazuri, lakini nililowafunga Stand United, msimu uliopita ndio bao langu bora,” alisema Chama.

Mchezaji huyo kwa sasa yupo kwao Zambia akisubiria hali ya janga la ugonjwa wa Corona lipungue na shughuli za michezo kurejea.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles