CHAINZ AMNUNULIA MAMA YAKE NYUMBA NYINGINE

0
500

NEW YORK, MAREKANI


MSHINDI wa tuzo za Grammy nchini Marekani, Tauheed Epps ‘2 Chainz’, amemnunulia mama yake nyumba ya pili baada ya mafanikio yake ya muziki kuwa makubwa.

Msanii huyo kutoka Atlanta, alimnunulia mama yake nyumba ya kwanza mwaka 2012.

“Mwaka 2012 nilimnunulia mama yangu nyumba kutokana na kiasi cha fedha nilichokuwa nikikipata wakati huo, sikuwa na uhakika kama mafanikio yangu yangekuwa makubwa mwaka huu, lakini sasa kipato changu kimezidi kukua.

“Sina ambacho naweza kumfanyia mama yangu nikafikia yale aliyonitendea, hivyo atakuwa anafurahia mafanikio yangu, nimeona bora nimnunulie nyumba nyingine kwa kuwa nampenda sana,” aliandika 2 Chainz kwenye ukurasa wake wa Instagram.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here