29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Chadema yamshtaki JK Umoja wa Mataifa

Mallya-wa-Chadema--620x309NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MWANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mallya, amesema wamemshtaki Rais Jakaya Kikwete kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon, kutokana na kauli ya kuwatisha wanaotaka kulinda kura kwamba wataona.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu sheria inavyoruhusu wananchi wenye shughuli za aina gani wakae ndani ya mita 200 na wale wanaoruhusiwa kukaa nje ya mita 200.

“Kifungu cha sheria namba 104(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinaruhusu wale wenye shughuli za kisiasa kukaa umbali nje ya mita 200, lakini wale waliokuwa na shughuli nyingine wanaruhusiwa kuendelea na shughuli zao ndani ya mita 200.

“Rais Kikwete ana kinga ya kushtakiwa, kutokana na kauli yake ya kuwatisha wananchi tumeamua kumshtaki jumuiya ya kimataifa, leo (jana) tumemwandikia barua Ban Ki-Moon na nakala tumepeleka sehemu mbalimbali ikiwamo London, Umoja wa Afrika na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

“Kwakuwa Tanzania ni nchi mwanachama, ilikubali kuwekewa vikwazo, kuadhibiwa, sisi barua yetu inataka UN iingilie kati,” alisema Mallya.

Alisema wanaamini UN watamwelewesha Rais Kikwete aiachie NEC ifanye kazi yake.

Pia alisema wameiandikia barua NEC kutaka wataalamu wa kompyuta na wengine waruhusiwe kukagua mfumo wa kukusanya matokeo na kuhesabu kura, na kama hilo halitawezekana utumike mfumo wa zamani.

Akizungumzia amani, alisema ni tunda la haki, nao wanataka uchaguzi uwe wa haki na ndiyo sababu Chadema inahutubia amani, lakini hawawezi kunyamazia uvunjivu wa amani.

Akizungumzia kampeni, Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alisema leo Ukawa wanasimamisha kufanya kampeni nchi nzima kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Emmanuel Makaidi wa chama cha NLD katika viwanja vya Karimjee.

Alisema kampeni hizo ni za wagombea wote, kuanzia udiwani hadi urais na viongozi wote watakuwapo katika kuuaga mwili wa kiongozi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles