28.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 25, 2021

CHADEMA WATUPWA NJE UBUNGE EALA, WAAPA KWENDA MAHAKAMANI.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana usiku wamewachagua wajumbe 7 wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania huku wagombea wawili wa CHADEMA wakitupwa nje baada ya kupigiwa kura za 'HAPANA', utaratibu uliopitishwa na Spika Job ndugai baada ya mvutano wa takribani saa moja juu ya jinsi ya kuwapigia kura wagombea hao wawili wa CHADEMA ambao ni Lawrence Masha na Ezekiel Wenje.

Kabla yakupiga kura palitokea mabishano ya kikanuni juu ya wagombea hao wa CHADEMA yaliyosababishwa na chama hicho kuweka wagombea wawili pekee huku nafasi kwa ajili ya chama hicho zikiwa mbili pia. Suala hilo lingewalazimu wapiga kura kupiga kura za kuwakubali wagombea hao hata kama hawawataki.

Hata hivyo, Spika Job Ndugai aliamua kura zipigwe, lakini kwa kundi la wagombea wa CHADEMA akaelekeza kuwa wapiga kura wana uhuru wa kuweka alama ya 'tick' kama wanamkubali mgombea au alama ya 'X' kama hawamkubali.

Awali wagombea wote walitumia utaratibu wa kujieleza mbele ya wabunge kabla ya zoezi la upigaji kura.

MATOKEO:

Kwa upande wa CCM, walioshinda ni 
1. Fancy Nkuhi
2. Happiness Legiko 
3. Maryam Ussi Yahya 
4. Dkt Abdullah Makame 
5. Dkt Ngwaru Maghembe 
6. Alhaj Adam Kimbisa

Kwa upande wa CUF aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo. CUF ilikuwa na nafasi ya mjumbe mmoja tu.

Baada ya matokeo hayo, Mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni, Mhe Freeman Mbowe alizungumza kuwa hawakubaliani na matokeo na wataenda Mahakamani kupinga matokeo hayo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,099FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles