31.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

Chadema kupeperusha bendera nusu mlingoti

Grace Shitundu, Dar es salaam

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa salamu za pole kufutia kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamini Mkapa, na kuwataka viongozi waliopo na wajao kuyaenzi mambo manne muhimu ambayo aliyaandika katika kitabu chake.

Pia chama hicho kimetangza kushusha bendera zake zote nusu mlingoti kwa kuwa Mkapa alikuwa ni Rais wa Watanzania wote.

Akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi zao zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema alisema wamezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa na kuwataka viongozi kumuenzi kwa vitendo.

Alisema Mkapa ameacha  wosia katika kitabu chake alichoandika mwaka uliopita na ni vizuri  akaenziwa kwa kuyaishi maandishi yake.

“Kuna mambo manne ambayo Mkapa aliandika katika kitabu chake ambayo sisi tungeomba watawala wafuate moja ni kuwa na tume huru ya uchaguzi kuenzi wosia wake  

“ Mzee Mkapa katika kitabu chake aliandika kuwa kuna haja ya kuwa na tume huru ya Uchaguzi kama watawala wanataka kuenzi maisha yake na kuenzi wosia wake wakatekeleze hilo sasa kwa sababu aliandika kwamba nchi hii inauhitaji wa Tume Huru ya uchaguzi na sasa tunaeleka tunaingia kwenye uchaguzi.

Mrema alisema jambo la pili ambalo wangependa viongozi walizingatie ni kudumisha diplomasia na uhusiano na nchin nyingine.

“Tungependa watawala walizingatie kama wosia wake, Mzee Mkapa kwanza aliasisi diplomasia ya Uchumi wote tunakumbuka, kwa sasa  nchi yetu imerudi nyuma kwenye upande wa diplomasia, viongozi wetu hawafanyi diplomasia aliyofanya Mwalimu Nyerere, aliyofanya Mzee Mwinyi  diplomasia aliyofanya Mzee  Mkapa.

“Kwa hiyo kama wanataka kumuenzi kuna haja ya kuenzi diplomasia mahusiano, viongozi wetu watoke wazungumze na viongozi wengine, sisi sio kijiji, sisi ni sehemu ya dunia,” alisema Mrema.

Pia Mrema alisema kuwa majuto ya Mkapa kuhusu mauaji ya yaliyofanyika Zanzibar mwaka 2001 akiwa kama Rais yakawe funzo kwa viongozi wengine waliopo na wajao.

“Mkapa mwaka jana ikiwa ni mwaka mmoja tu kabla hajafariki kwenye kitabu chake aliandika kwamba katika utawala wake kitu kinachomtesa na kinachomuumiza ni kuhusu mauaji yaliyofanyika Zanzibar, damu iliyomwagiza kule Zanzibar akawa amejutia hivyo viongozi wote watambue kuna maisha baada ya kutoka madarakani, tusifanye mambo halafu baadae tuje kujuta, tufanye mambo mema kwa wananchi wetu,” alisema Mrema. 

Mrema alisema jambo la nne ambalo wanapenda viongezi wengine waige ni kuwa Mkapa alikuwa tayari kuchukua mambo mema hata kutoka kwa vyama ya upinzani.

“Nitawakumbusha watanzania kwamba Mzee Mkapa aliondoa kodi iliyokuwa inaitwa kodi ya kichwa, hii ilikuwa sera ya chadema na tuliposhinda Halmashauri ya Karatu tulianza kuitekeleza kule karatu tukafuta ile kodi ya kichwa ambayo wananchi walikuwa awanasumbuliwa sana. 

“Kwa hiyo iwe funzo kwa viongozi wetu wa sasa na wajao kwamba kuchukua mambo mema kwa manufaa ya wananchi wetu ni jambo nzuri ambali Mzee Mkapa ametuachia” 

Aliongeza kusema “Kwa hiyo kwa kifupi sana hayo ndio mambo ambayo tungependa kusema kwa niaba ya chama kuhusu msiba huu wa Taifa letu, na kama watanzania na sisi Chadema tutaendelea kuomboleza na kufurahia maisha yam zee mkapa na kukumbuka haya mambo manne aliyotuachia,” alisema Mrema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles