24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

CHADEMA, ACT WAKUBALIANA RASMI UCHAGUZI BUYUNGU

Na ANDREW MSECHU

-DAR ES SALAAM

BAADA ya mazungumzo na ushauriano wa viongozi wa pande zote mbili, vyama vya ACT Wazalendo na Chadema hatimaye   vimekubaliana katika maeneo sita kwenye uchaguzi wa ubunge Buyungu na madiwani kata 77.

Taarifa iliyotolewa jana na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kampeni na Uchaguzi wa ACT Wazalendo, Mohammed Babu pamoja na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi, ilieleza kuwa vyama hivyo vimekubaliana kuwa ACT  kitaiachia Chadema Jimbo la Buyungu na kushiriki kwenye kampeni huku Chadema kikiachia ACT Kata ya Gehandu (Hanang) na kushiriki kwenye kampeni.

“Chadema kitaiunga mkono ACT Wazalendo kwenye kata ambazo ACT pekee kimegombea,  ACT Wazalendo kitaiunga mkono Chadema kwenye kata ambazo Chadema pekee kimegombea.

“Wagombea wa vyama vyote kwenye kata zilizosalia wataruhusiwa kuendelea na kampeni. ACT Wazalendo na Chadema vitashirikiana kukabiliana na hujuma kwenye kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles