Celine Dion apiga shoo baada ya kufiwa na mama yake

0
542

MIAMI, MAREKANI

MKALI wa sauti Celine Dion, mwishoni mwa wiki iliopita alipiga shoo kwa hisia kali ikiwa ni siku moja baada ya kufiwa na mama yake Therese Tanguay.

Kifo cha mama wa msanii huyo kilitokea Ijumaa, lakini msanii huyo alipiga shoo Jumamosi huku akiwaambia mashabiki kwamba upendo wake kwao umemfanya kuwa na nguvu ya kufanya shoo hiyo.

Hata hivyo, mbali na kuwa na nguvu ya kuwaburudisha mashabiki zake, lakini kuna wakati alijikuta akitokwa na machozi kwa kumkumbuka mama yake ambaye amepoteza maisha huku akiwa na umri wa miaka 92.

“Ninaendelea vizuri baada ya kumpoteza mama yangu, hata familia kwa ujumla ipo sawa, najua kila mmoja ana taarifa ya kufariki dunia kwa mama yangu, familia ilipata nafasi ya kumuaga kwa pamoja kabla ya kupoteza maisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here