30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Cecil Mwambe: Natinga bungeni

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

SIKU chache baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kueleza kutotambua barua ya Chadema kuhusu uko- mo wa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe, mwanasiasa huyo amesema atatinga bungeni na kwamba atakaa upande wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Jana Jioni MTANZANIA Jumamosi lilifua- tilia kuona kama Mwambe ataingia bungeni lakini hakuonekana.

Mwambe ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo la Ndanda, Februari 15 mwaka huu alitangaza kujivua uanachama wa Chadema akiwa ofisi ndogo za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, Dar es Salaam na kupokewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho tawala, Humphrey Polepole.

Mwanzoni mwa wiki hii, Spika Ndugai aliwaeleza wabunge kuwa alipokea barua ya Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kwamba Bunge lisimtambue Mwambe kama mbunge na asipate stahiki zozote.

“Lakini barua yenyewe jinsi ilivyoandikwa ni fupi, niwasomee tu. Anasema; “Bwana Cecil Mwambe ali- kuwa mbunge wa jimbo la Ndanda aliyekuwa amed- haminiwa na Chadema hata hivyo Februari mwaka huu alitangaza kupitia vyombo vya habari kwamba amehama chama hicho.

“Hivyo basi kwa mujibu ibara ya 7 (1 F ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekoma kuwa mbunge na ameacha kiti chake katika Bunge, kwa hiyo Bunge lisiendelee kumpatia sitahiki zozote.”

Ndugai alisema; “sasa namshangaa Mnyika kwa sababu hayo maneno anayosema alipaswa aambatan- ishe na barua ya Mwambe inayothibitisha haya anay- osema, hakuambatanisha.

“Pili, mimi sina barua ya Mwambe ya kusema kwamba kaacha ubunge kwa hiyari yake mwenyewe, na kama ni chama hiki (Chadema) kimechukua hat- ua, sina viambatanisho vinavyoonyesha vikao halali vilivyofanya maamuzi hayo, kwahiyo hii barua haina maana, haina mantiki.

“Nichukue nafasi hii kuwaambia wabunge wote ‘including’ wabunge wa Chadema na wengine wa- naotishwatishwa huko msibabaike, msiwe na wasiwa- si, mnaye Spika imara atawalinda mwanzo mwisho, habari ya ukandamizaji na ubabaishaji hauna nafasi, fanyeni kazi zenu kwa kujiamini, mmeaminiwa na wa- nanchi, fanyeni kazi zenu wala msiwe na wasiwasi.”

KAULI YA MWAMBE

Jana akizungumza na redio moja, Mwambe alise- ma tayari yuko Dodoma kusikiliza wito wa Ndugai kwa kuwa alitakiwa kuendelea na shughuli zake za kibunge.

Alipoulizwa kuwa atakuwa mbunge wa chama kipi kwa sababu tayari alishajiuzulu uanachama wa Chadema, naye alihoji kwani awali alikuwa mbunge kwa chama kipi?.

Katika hilo alisisitiza kuwa ataendelea kuwa Mbunge wa Ndanda kupitia Chadema.

Kuhusu kama ataendelea kuwa mwanchama wa Chadema, alisema: “Nilijiuzulu uanachama wa Chadema, nikaacha ubunge mheshimiwa spika amenitaka nije nimalizie muda wangu uliobaki naweza kuwa si muumini wa Chadema lakini mwisho wa siku nimerudi bungeni kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na spika.

“Lakini nitaenda CCM kama nilivyosema wakati najiuluzu na nitagombea ubunge kupitia CCM,”alisema.

“Kwa sasa nimetii wito wa mimi ni mtiifu nimetii wito wa spika nitakaa upande wa upinzani ambayo in- aongozwa sasa na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Rwakatare sio ile ya Freema Mbowe na nimeshaku- tana na Rwakatare amenipa baraka zote kuwa niend- elee nikamalizie muda wangu uliobaki,”alisema.

Akizungumzia kuhusu taarifa kwamba aliendelea kupokea mshahara wa ubunge pamoja na kujiuzulu, alisema si kweli na walioeneza taarifa hizo walipoto- sha kwa makusudi.

“Mimi nasema spika alikuwa hanilipi mshahara na mshahara wangu wa mwisho nimepokea Februari 15 mwaka huu ambao niliupokea Machi wanaposema niliendelea kulipwa si kweli wameamua kupotosha lakini nilipotangaza kujiondoa pale kila kitu changu kilisitishwa,”alisema Mwambe.

Uamuzi wa Spika kumrudisha Mwambe umezua mjadala mkali uliowaibua wanasheria ambao wame- onekana wazi kutounga mkono hoja za Spika hasa kwa kuzingatia kwamba Mwambe alitangaza kujion- doa yeye mwenyewe na si Chadema kumfukuza.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,348FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles