25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

CCTV zanasa walarushwa mizani

Na Mwandishi wetu-Iringa

WATU tisa wameshikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi nchini kwa mahojiano baada ya kubainika kufanya vitendo viovu katika mizani hapa nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya ujenzi, Elius Mwakalinga, alisema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi, lililofanyika mkoani Iringa.

Pamoja na mambo mengine, alisema wizara itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wasafirishaji ambao watakiuka sheria ya udhibiti wa uzito wa magari ya mwaka 2016.

“Toka tuanze mfumo tumeshawashika watu 11 na bado tunaendelea kufuatilia ili tuwashike zaidi na hatua

kali zitachukuliwa ili kukomesha vitendo vya uhujumu katika mizani,” alisema Mwakalinga.

Alisema hatua hiyo imekuja baada ya sekta hiyo kuanzisha utaratibu wa kufuatilia utendaji kazi wa mizani kwa saa 24 kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kamera za CCTV kuongeza uwazi na uwajibikaji na kudhibiti rushwa.

Mwakalinga alisema sekta hiyo imeanza mchakato wa ununuzi wa gari kwa mfumo wa kusimamia miundombinu ya barabara kwa ufanisi, weledi na kwa gharama nafuu ikiwa na lengo la kuhakikisha kazi za ukaguzi wa barabara zinafanywa kwa ufanisi.

“Gari hilo litakuwa la kisasa na lenye mionzi itakayowezesha kukagua mtandao wote wa barabara nchini ndani ya mwezi mmoja na kutoa majibu ya ubora na mapungufu ya barabara kuanzia hatua za awali za ujenzi hadi mradi utakapokamilika,” alisema Mwakalinga.

Katika kuhakikisha Tanzania inapata wakandarasi wazawa na wenye uwezo wa kujenga na kusimamia miradi mikubwa, alisema sekta hiyo imepeleka wataalamu 33 kwenye miradi mbalimbali ili kuleta mapinduzi sekta za ujenzi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, aliipongeza sekta hiyo kwa kuandaa baraza hilo na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ambayo ina lengo la kukuza uchumi wa nchi.

“Nichukue fursa hii kuipongeza sekta hii kwa kuandaa baraza hili na mikakati ya kiutekelezaji ambayo mmejiwekea, naamini kupitia mipango yenu nchi hii itapata wataalamu wengi zaidi ambao wataweza kusaidia kuleta maendeleo ya taifa hili,” alisema Hapi.

Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi la siku mbili ambalo lina wajumbe zaidi ya 100 limekutana kupitia na kujadili taarifa za utekelezaji wa sekta, mafanikio pamoja na changamoto za sekta hiyo ili kufikia maamuzi yanayohusu sekta ya ujenzi na taasisi zake. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles