23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YATOA SIRI YA USHINDI UCHAGUZI MDOGO

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


 

Humphrey-PolepoleCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mageuzi ya kiuongozi yaliyofanywa katika chama hicho na utendaji mzuri wa Serikali, ndiyo siri ya ushindi katika uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili iliyopita.

Katika uchaguzi huo, CCM ilishinda ubunge wa Dimani Zanzibar na udiwani katika kata 19 kati ya 20 zilizofanya uchaguzi Januari 22, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole, alisema mageuzi ya kiuongozi, kimfumo na kiutawala yamekirejesha chama hicho kwa wanachama ambayo ndiyo msingi wa uanzishwaji wake.

“Kuna watu walikuwa wanatutabiria giza mwaka 2020, lakini kwa ushindi huu tunauona mwanga mkubwa unaotufanya tufanye kazi zaidi kuwaletea maendeleo Watanzania.

“Licha ya hujuma, upotoshwaji, kubezwa kwa CCM na kazi nzuri inayofanywa na Serikali iliyo chini ya Rais Dk. John Magufuli, lakini ndani ya mwaka mmoja tunaona ahadi nyingi zina uhalisia, kuna mapambano makubwa dhidi ya rushwa na ufisadi, utoaji elimu bure, uwajibikaji na huduma za kiuchumi,” alisema Polepole.

Chama hicho pia kimeitaka Serikali kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha mianya yote ya wakwepa kodi inazibwa ili fedha zote zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

Aidha Polepole aliikumbusha Serikali kuweka msisitizo katika maeneo mengine yaliyoahidiwa kama vile kutenga asilimia 10 ya mapato ya Serikali za mitaa kwa wanawake na vijana ili wapate fursa za mitaji na mikopo.

Katika hatua nyingine, chama hicho kimekitaka Chama cha Wananchi (CUF) kitafute mchawi wa kushindwa katika uchaguzi huo na kuacha kutoa visingizio.

“Tumekuwa tukilaumiwa sana na CUF, lakini matokeo ya Dimani yamedhihirisha kwamba tatizo ni wao wenyewe, tumefanya utafiti mdogo uchaguzi wa 2015 Dimani walipata kura 2,300. Lakini katika uchaguzi mdogo kimepata kura 1,200 CCM kilipata kura 4,400 na katika uchaguzi huu tumepata zaidi ya kura 4,800. Hivyo CUF kimtafute mchawi na hasa hasa Zanzibar,” alisema.

Akizungumzia uchaguzi wa ndani ya chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, alisema watahakikisha wanawapata viongozi bora wanaoakisi matarajio na hitaji la Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles