29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yatoa agizo kwa watendaji wa Serikali

IS-HAKA OMAR-TUNDURU

MLEZI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk. Abdullah Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewataka viongozi na watendaji wa chama na Serikali  wilayani Tunduru kufanya mikutano ya ndani ya mara kwa mara na wananchi ili kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Alisema kufanya mikutano hiyo kutasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi kwani watapata uelewa mpana wa  mambo mbalimbali ya maendeleo yanayotekelezwa na Serikali.

Agizo hilo amelitoa jana wilayani hapa katika ziara yake alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Tunduru, watendaji wa halmashauri  pamoja na wazee wa CCM.

Alisema Serikali imetekeleza ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kuwapelekea huduma za kijamii zikiwemo za afya, elimu, miundombinu ya barabara, mawasiliano, uvuvi, kilimo na miundombinu ya usafiri wa anga.

Pamoja na hali hiyo Dk. Mabodi pia aliutaja mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF), unaotekelezwa kwa awamu ya tatu sasa umekuwa ni sehemu ya mafanikio kwa wananchi kwa kuwezeshwa kiuchumi ambao wengi wao wamekuwa wakijipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM, alisema kuwa kutofanyika kwa mikutano ya mara kwa mara na wananchi husababisha kuibuka kwa malalamiko kwa kuhisi kero zao zimekosa utatuzi.

“Lengo la ziara yangu ni kuimarisha hali ya kisiasa kwa chama (CCM) kwa kuangalia maeneo mbalimbali ikiwemo kueneza itikadi ya ujamaa na kujitegemea, kuhakikisha rasilimali za chama zikiwemo majengo ya ofisi na mikutano vinakwenda kwa hadhi ya CCM.

“… pamoja na kuhamasisha uendelezaji wa madarasa ya itikadi, kufungua mashina na kueleza muelekeo wa sera za maendeleo zinazotekelezwa na Chama Cha Mapinduzi,” alisema Dk. Abdullah.

Alisema pia lengo lingine ni kuhakikisha maandalizi ya utekelezaji wa Ibara ya 5 ya Katiba ya CCM ya mwaka ya mwaka 1977 toleo jipya la mwaka 2017 la kuhakikisha CCM, inashinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles