31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CCM YAONYA WANAOCHAFUA WENZAO MITANDAONI

Na TIMOTHY ITEMBE


WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Tarime   wameonywa kuacha tabia ya kuwachafua  wagombea wenzao katika mitandao ya  jamii katika kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani wa chama.

Onyo hilo lilitolewa  na Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamis Mukaruka ambaye alisema watakaobainika kujihusisha na tabia hiyo hatua za  nidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

“Chama hakitawavumilia wanachama na wagombea au wanachama wowote ambao wanatumia njia ya kuwachafua wenzao wanaogombea kwenye mitandao ya  jamii.

“Niseme kwa sasa tuko makini na watakaobainika watachukuliwa hatua za  nidhamu,” alisema.

Aliwataka wanachama waliokisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu   wa mwaka 2015 kutopoteza muda wao kwa kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa wataenguliwa.

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Tarime, Mathias Lugola aliwasihi wanachama kuendelea kujitokeza kuwania nafasi za uongozi wa jumuiya hiyo.

Nafasi hizo ni mwenyekiti, katibu wa siasa na uenezi, wajumbe wa halmasghauri kuu ya wilaya nafasi 10, wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa nafasi tatu na wajumbe wa mkutano mkuu mkoa nafasi tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles