23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

CCM yampongeza Dk. Bashiru kusimamia maadili 

Mwandishi Wetu-Morogoro

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Morogoro, kimewataka wanasiasa kutambu kuwa siasa za ukabila, udini, rangi au ukanda na majimbo hazina nafasi katika ujenzi wa Taifa.

Kutokana na hali hiyo, kimepongeza uamuzi wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally kwa kuwa kingozi wa mfano na mwenye kusimamia maadili, miiko ya chama hicho na kuleta umoja na mshikamano.

Hayo wamesemwa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza katika mahafali ya wahitimu wa vyuo vikuu mjini hapa.

Alitahadharisha ndimi za viongozi wa serikali, vyama vya vya siasa kuwa vinahitaji kuchuja maneno kabla ya kutoka kwa umma.

“CCM Mkoa wa Morogoro, tunasifu na kupongeza  msimamo thabiti ulioonyeshwa na Dk. Bashiru Ally kwa kuthubutu kukemea baada ya kujitokeza sintofahamu ya matamshi yenye dhihaka ya ukabila na hapo hapo kuwakanya wanaofanya hivyo,” alisema Shaka.

Alisema  matamshi ya dhihaka za ukabila na dini zina makali yenye ncha hatari kuliko za panga lilinolewa na kupata makali au mishale yenye ncha na sumu kali.

“Tunampongeza Dk. Bashiru kwa kusimamia kwake miiko, maadili falsafa na sera za chama kwa vitendo,licha ya kuwepo ombwe la kufanyika mafunzo ya itikadi ya chama, vijana kutofunzwa miiko ya utawala, utii wa maadili ya uongozi, nidhamu na mwenendo wa siasa safi, niwaombe vijana wenzangu tusiwe wavivu wa kujisomea machapisho na vitabu.

“Tukumbuke vijana wenzangu  bado yapo machapisho na vitabu vyenye miiko, maadili na mwelekeo wa siasa ya chama na uongozi bora .Ni suala la mtu kutenga wakati wake na kuamua kujisomea ili ajijengee maarifa,  heshima na utii,” alisema Shaka.

Alisema hata kwa kusikiliza kwenye radio au kuangalia luninga  hotuba za viongozi kama  Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Sheikh Abeid Karuma, Ali Hassan Mwinyi ,Rashid Kawawa, Sheikh Thabiti Kombo na baadae za kina Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na sasa Dk. John Magufuli ni zaidi ya kusoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,”alisema Alisema sifa ya utambuzi wa dhana za masuala ya utawala, uongozi na siasa safi isitokane na mtu kujiona amefikia elimu ya Chuo kikuu peke yake ikamtosha

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles