27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yamlilia Teddy Mapunda

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kimemtaja marehemu, Teddy Mapunda kuwa amekuwa mdau muhimu na mshirika kinara aliyeshirikiana vyema na vyombo vya habari kwa ukaribu mno hivyo Taifa limempoteza Mtanzania makini aliyejawa hisia za uzalendo na utaifa.

Pia marehemu Teddy atakumbukwa kwa tabia zake za kuoenda ucheshi, huruma na upendo akiwa si mwenye majivuno, asiyedharau wenzake lakini pia hakupenda kujikweza na kuwakoga watu.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka.

Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari kabla ya mazishi kufanyika nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach, Dar es Salaam, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Katibu Mkuu wa (CCM), Daniel Chongolo amemtaja Teddy kuwa alikuwa Mtanzania aliyependa sana habari muhimu za kitaifa ziwafike wananchi wanaoishi vijijini na mijini  kwa haraka na usahihi .

Shaka amesema alikuwa na kiu  na mbinu za uwezeshaji wa kutosha ili habari ziweze kuwafika  wananchi aidha wanaoishi mijini na vijijini na kuitangaza nchi yake hasa alipokuwa akifanyakazi  katika mbuga ya wanyama ya Taifa Serengeti. 

“Hayati Teddy sifa yake kubwa ilikuwa ni unyenyekevu, ucheshi  na mwenye  moyo wa huruma . Alikuwa ni mtanzania mzalendo, mtaifa na mchapakazi aliyependa kuona umoja wa kitaifa ukidumu nchini,” amesema Shaka.

Amesema atakumbukwa sana kwa tabia yake na mwenendo bora na adilifu kwani hakuwa mtu mbabaishaji na asiyevunja wala kutotimiza miadi mnapowekeana ahadi kwani aliheshimu wakati.  

“Tuige maisha aliyoishi mwenzetu hapa duniani kwani hakuwa mtu wa majivuno. Hakuwa akivunja miadi pia hakupendelea wala kuwa na roho ya korosho. Mikono yake haikuwa kama ile ya birika. Badala yake alipenda kuwasaidia  wenzake kila alipoweza na kuitazama jamii,” ameeleza .

Aidha, shaka alisema ni watu wachache mno duniani pale wanaopata nafasi hujikuta wakizitumia vibaya kuwakomoa wenzao , kuwanyanyasa na kuwapuuza wengine jambo ambalo katika maisha ya Teddy ilikuwa ni kinyume  na hivyo. 

Katibu huyo wa NEC Itikadi na Uenezi aliwahimiza watu wengine kutambua kuwa wanadamu katika dunia wana  safari fupi hivyo  isiwaghilib badala yake kila mmoja ajijue iko siku ataondoka duniani na kurudi kwenye vumbi. 

Hivyo basi shaka alisema chama cha Mapinduzi kinatuma  salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kumuomba  Mungu awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu  kwao cha  msiba na maombolezo ili mungu amuweke mahali pema peponi .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles