29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

CCM YALALAMIKA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Dialo amesema miongoni mwa matatizo ambayo watumishi wengi wanaostaafu au kuondolewa katika nafasi wanazoteuliwa na Rais ni kukiuka kiapo chao cha kutunza siri, anaripoti Benjamin Masese.

Dk. Dialo alisema wapo watumishi wengi hususan wa kuteuliwa wakiwamo  mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala na wengine  wamekuwa wakitoa siri  walizopata wakati wakitumikia nafasi zao kitendo ambacho kinakiuka kiapo chake.

Kauli hiyo aliitoa  hivi karibuni alipozungumza na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mwanza walioteuliwa  Julai 28, mwaka huu na Rais Dk. John Magufuli  huku akiwataka   waliostaafu kwa umri   na walioondolewa katika nafasi zao kuendelea kutunza siri za Serikali.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,310FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles