29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

CCM, Ukawa kazi ipo

mtanzaniadaily.inddNa Ramadhan Hassan, Dodoma

MATOKEO ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji yaliyotangazwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, yameonyesha vyama vya upinzani vinazidi kuibana CCM katika maeneo ya mjini.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana, wapinzani wamepata asilimia 33 mijini na 19 vijijini.
Wakati hali ikiwa hivyo, CCM yenyewe imezidi kujiimarisha zaidi katika maeneo ya vijijini ambako imeibuka na ushindi wa asilimia 80.58.
Ushindi huo wa CCM, umekuwa tofauti na mwaka 2009 ambako iliibuka na ushindi wa jumla wa asilimia 91.72 na upinzani asilimia 8.28.
Akitangaza matokeo ya jumla mjini Dodoma jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi(TAMISEMI), Khalist Luanda, alisema CCM imeshinda uchaguzi huo kwa asilimia 80.58.
Alisema CCM imepata vijiji 7,290 sawa na asilimia 80.58, huku ikichukua mitaa 2,116 sawa na asilimia 67.90.
Luanda alisema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepata vijiji 1,248 sawa na asilimia 13.79 na mitaa 753, sawa na asilimia 25.63.
Alisema Tanzania ina vijiji 9,047 na mitaa 3,078.
Luanda alisema Chama cha Wananchi (CUF) kimepata vijiji 949 sawa na asilimia 4.22 na mitaa 235 sawa na asilimia 7.27, wakati Chama cha Tanzania Labour (TLP) kimepata vijiji viwili na mtaa mmoja ambavyo ni sawa na asilimia 0.02.
“Chama cha NLD kimepata vijiji viwili sawa na asilimia 0.02 na UDP kimepata vijiji vinne,” alisema.
Alisema katika ngazi ya mitaa, Chama cha NCCR-Mageuzi kimepata mtaa mmoja sawa na asilimia 0.25, CUF mitaa 8 sawa na asilimia 7.27, ACT-Tanzania mitaa 9 sawa na asilimia 0.03, UMD mtaa mmoja, UDP mtaa mmoja sawa na asilimia 0.03 na NRA kimepata mtaa mmoja,” alisema.

ARUSHA

Luanda alisema Halmashauri ya Arusha yenye vijiji 64, CCM imeshinda 56, huku Chadema ikipata vijiji 8, wakati Halmashauri ya Meru yenye vijiji 79, CCM imeshinda 51 na Chadema 28.
Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ambayo ina vijiji 62, CCM imeshinda vyote, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Longido ambayo ina vijiji 49, CCM ilipata 48 na Chadema kimoja.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro yenye vijiji 72 vyote vimechukuliwa na CCM.

DAR ES SALAAM
Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye mitaa 188, CCM imepata 139, Chadema 34 na CUF 15.
Luanda alisema Halmashauri ya Temeke yenye mitaa 172, CCM imepata 115, Chadema 27, huku CUF ikipata 30.

DODOMA
Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma yenye mitaa 17, CCM imeshinda yote.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa yenye vijiji 92, CCM imepata 71, Chadema viwili na CUF 19, wakati Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa yenye vijiji 96 vyote vimechukuliwa na CCM.
Kwa upande wa Kongwa yenye vijiji 82, CCM imeshinda vyote na huko Chemba yenye vijiji 107, CCM imepata vijiji 73, Chadema 9 na CUF 14.
Katika Wilaya ya Chamwino yenye vijiji 39, CCM imeshinda 38 na Chadema kimoja wakati Bahi yenye vijiji 59, CCM imepata 53, Chadema 5 na ADC kimoja.

GEITA
Huko mkoani Geita katika Halmashauri ya Bukombe yenye vijiji 48, CCM imeshinda 29, Chadema 18 huku Halmashauri ya Chato yenye vijiji 115, CCM imepata 88, Chadema 27, wakati Halmashauri ya Geita yenye vijiji 142, CCM imepata 99 na Chadema 32.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe yenye vijiji 18, CCM imeshinda 17 na Chadema kimoja.
Katika Halmashauri ya Nyang’wale yenye vijiji 18, CCM imepata 17 na Chadema kimoja.

IRINGA
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yenye mitaa 181, CCM imepata 126, Chadema 54 na CUF ikipata mmoja, wakati Mufindi yenye vijiji 39, CCM imepata 35 na Chadema kimoja.
Halmashauri ya Kilolo ambayo ina vijijini 81, CCM imepata 78 na Chadema vitatu.

KAGERA
Katika Halmashauri ya Biharamulo yenye vijiji 77, CCM imepata 41 na Chadema 36, wakati katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba yenye vijiji 94, CCM imepata 79 na Chadema 10.
Katika Manispaa ya Bukoba yenye mitaa 66, CCM imeshinda 34, Chadema 30 na CUF miwili.
Karagwe yenye vijiji 77, CCM imepata 53 na Chadema 19 na huko Kyerwa yenye vijiji 95, CCM imeshinda 51 na Chadema 14.
Misenyi yenye vijiji 77, CCM imepata 64, Chadema 12 na Mulema yenye vijiji 166, CCM imeshinda 91 Chadema 70, wakati Halmashauri ya Ngara yenye vijiji 66, CCM imeshinda 61 na Chadema vinne.

KILIMANJARO
Manispaa ya Moshi yenye mitaa 55, CCM imeshinda 28, Chadema 27; Hai vijiji 54, CCM imeshinda 33, Chadema 21; Siha yenye vijiji 60, CCM imeshinda 52, Chadema 8; Same vijiji 96, CCM imeshinda 78, Chadema 17; Mwanga yenye vijiji 72, CCM imeshinda 66, Chadema 6 na Rombo kati ya vijiji 55, CCM imeshinda 33 na Chadema 22.

MBEYA
Halmashauri ya Mbeya yenye mitaa 179, CCM imeshinda 103, Chadema 74 na NCCR-Mageuzi mitaa miwili; Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya yenye vijiji 72, CCM imepata 52, Chadema 20; Chunya yenye vijiji 69, CCM imepata 66 na Chadema vitatu; Mbarali yenye vijiji 93, CCM imepata 78 na Chadema 15; Kyela vijiji 92, CCM imepata 79 Chadema 13, wakati Ileje yenye vijiji 70, CCM imepata 53, Chadema 15 na TLP kijiji kimoja.
Halmashauri ya Wilaya ya Momba yenye vijiji 86, CCM imevuna 77 na Chadema 9 na Busokelo yenye vijiji 56, CCM imepata 51 na Chadema 5.

MWANZA
Jiji la Mwanza lenye mitaa 174, CCM imepata 97, Chadema 70 na CUF 7; Ilemela yenye mitaa 168, CCM imeshinda 106, Chadema 62; Kwimba yenye vijiji 31, CCM imepata 26 na Chadema 5, wakati Magu yenye vijiji 82, CCM imeshinda 51 na Chadema 27.
Misungwi yenye vijiji 74, CCM imeshinda 63 na Chadema 10; Ukerewe yenye vijiji 76, CCM imeshinda 27 na Chadema 47; Sengerema yenye vijiji 36, CCM imeshinda 33 na Chadema 3.
Luanda alisema mikoa iliyofanya vizuri katika uchaguzi huo ni Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Dodoma, Katavi, Arusha, Kagera, Mbeya na Singida.
Hata hivyo, alisema uchaguzi huo ulikuwa na dosari katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Pwani ambayo kuna maeneo katika baadhi ya wilaya zake hayajafanya uchaguzi na kwingine utarudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles