29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

CCM Ubungo yabariki safari ya JPM Ikulu

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja ameongoza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, kujaza fomu za kumdhamini mgombea urais wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.

Rais Magufuli amechukua fomu ya kuwania tena urais kwa kipindi cha pili jana jijini Dodoma na ameanza kusaka wadhamini 250 mikoani kama utaratibu wa CCM unavyoelekeza.

Taarifa ilitolewa leo na Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ubungo, Mbaruku Masudi, ilieleza kuwa wajumbe hao wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Ubungo , wameshiriki zoezi hilo kwa ngazi ya wilaya,
“Zoezi la udhamini kwa Wilaya yetu ya Ubungo, limehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Lucas Mgonja, Katibu wa CCM Wilaya Chifu Sylevester Yared pamoja na kamisaa wa chama Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori,” imeeleza taarifa hiyo.

Akizungumza na wajumbe hao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja, alisema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwao kwani wanaamini Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maoni na ataendelea kuifanyia mema Tanzania.

“Ubungo tunasema kwa kauli moja kwamba Magufuli anatosha, tunamwamini na tumemkubali na tunahakika atatuvusha tena. Miaka mitano ya kwanza hakika ametenda kazi kubwa na kila Mtanzania ni shuhuda nasi Ubungo alitupendelea kwa kuwa na miradi mikubwa ikiwamo Ubungo Inter Change pamoja na barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha kwetu ni heshima kubwa.

“Si hili tu hata ukiangalia miradi ya maji, ujenzi wa shule na zahanati pamoja na hospitali za wilaya nasi Ubungo ni sehemu ya wanufaika wakubwa wa miradi hii, kwa hakika Rais Magufuli ameitendea haki CCM na aliahidi na ametekeleza kila sekta kama ilani ya chama ilivyoelekeza,” amesema Mgonja.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles