30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Ubungo yaapa kurejesha majimbo, kata

Tunu Nassor – Dar es Salaam

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Ubungo kimewazi wazi mikakati yake ikiwamo kuhakikisha wanarudisha majimbo ya Ubungo na Kibamba pamoja na kata zote 14 katika Uchaguzi Mkuu utajaofanyika Oktoba mwaka huu ili yawe katika himaya yao.

Akizungumza katika semina elekezi kwa wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja alisema wameanza kujipanga kuanzia ngazi ya shina kwa kufanya vikao na viongozi wote.

Alisema wanafanya semina za viongozi mara kwa mara kuhakikisha kila mmoja anatekeleza majukumu kwa nafasi yake.

“Mikakati iliyopo ni kuhakikisha tunapata ushindi mkubwa katika nafasi ya urais, kurudisha majimbo yote mawili na kupata viti vyote 14 vya udiwani,” alisema Mgonja.

Alisema wamefanya ziara katika matawi 136 kuhakiki uhai wa chama ikiwa ni pamoja na kuondoa migogoro midogo baina ya wanachama ambayo huenda ingewatenga katika kipindi cha uchaguzi.

“Katika ziara hiyo tumeangalia pia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM  na kupokea kero mbalimbali za wananchi,” alisema Mgonja.

Aliongeza kuwa wanashukuru kupata msingi wa kuwa na wenyeviti wa serikali za mitaa 90 pamoja na wajumbe 450 wanaotokana na chama hicho.

“Tayari tuna msingi wa mkubwa wa ushindi kutoka kwa wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa ambapo sasa mitaa yote wanatokana na CCM,” alisema

Akizungumzia semina hiyo, Mgonja alisema viongozi hao wa mitaa wanatambulika na katiba ya nchi na katiba na sera ya CCM .

“Mtanatakiwa kusoma Ilani kwa kuwa kuna maelekezo kwenu yatakayowaongoza katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi,” alisema Mgonja.

Kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya hiyo, Chifu Sylvester Yaredi alisema semina hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuboresha weledi na ufanisi wa viongozi hao.

Alisema katika semina hiyo wamewajengea uaelewa katika suala la mahusiano mema kati yao na chama pamoja na maadili ya uongozi.

“Tunatarajia baada ya mafunzo haya ufanisi katika utendaji kazi utaongezaka mara dufu  baada ya kujua mipaka yao ya kazi,” alisema Yaredi.

Alisema wamejifunza miiko , wajibu na kipi wafanye na wasivyotakiwa kuviofanya wakati wa kutekeleza majukumu yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles