27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Mwanza yamtimua meya wa zamani Mwanza

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wa Mkoa, Saimon Mangelepa
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wa Mkoa, Saimon Mangelepa

Na PETER FABIAN,

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimewavua uanachama na kuwafukuza makada wake 100 akiwamo aliyewahi kuwa  Meya wa Jiji la Mwanza, Leonard Bihondo na mkewe Veronica Bihondo.

Watu hao wanadaiwa  kukisaliti na kuhujumu chama katika uchaguzi mkuu uliopita.

Hatua hiyo ilitangazwa juzi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mwanza baada ya vikao ngazi ya chini pia kufikia uamuzi huo.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wa Mkoa, Saimon Mangelepa, alisema   uamuzi   wa kuwavua uanachama na kuwafukuza kwenye chama ulianza kujadiliwa na kutolewa uamuzi kuanzia ngazi ya matawi, kata, wilaya na   mkoa.

“Kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 na toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93 (14)- (15)   leo wajumbe wametoa baraka zote na kuazimia kutekelezwa   adhabu hiyo kwa baadhi ya wanachama waliobainika kukisaliti chama kwenye uchaguzi mkuu 2015,”alisema.

Mangelepa alisema   makada na wanachama waliovuliwa na kufukuzwa    ni pamoja na Meya wa zamani wa Jiji la Mwanza, Bihondo ambaye anatoka Kata ya Isamilo, Wilaya ya Nyamagana.

Aliwania kugombea udiwani na kushindwa kwenye   kura ya maoni ndani ya chama lakini anadaiwa alihusika kumsaidia mgombea wa upinzani na kuishinda CCM.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles