27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

CCM kuwashughulikia wenyeviti watakaoshindwa kutatua kero za wananchi

EDITHA KARLO-KIGOMA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitawavua uanachama na kupoteza nafasi zao wenyeviti wa vijiji, mitaa na vitongoji nchini ambao watashindwa kusimamia malengo ya chama hicho ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi badala yake kutumia nafasi zao kujinufaisha.

Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Humphrey Polepole ametoa kauli hiyo akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Watendaji wa Mitaa na Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Kigoma.

Polepole alisema viongozi hao ndiyo kiunganishi kikubwa cha wananchi na serikali yao na wao wanajua kwa karibu matatizo yanayojitokeza.

Miongoni mwa maeneo ambayo amesema yamekuwa na tatizo kubwa ni pamoja na viongozi hao kutopatikana wananchi wanapokuwa na shida hasa kupata barua kwa ajili ya utambulisho kwenda maeneo mbalimbali, kutofanyika kwa vikao lakini pia kutosomwa kwa taarifa za mapato na matumizi.

“Kwa sasa tumeamua tunarudi kwenye misingi na asili ya CCM ya kuwatumikia wananchi, kama kiongozi anaona hatoshi na hawezi kasi ya Mwenyekiti wa Taifa Rais John Magufuli atupishe mapema, vinginevyo tutaondoa viongozi wote wa mitaa na kuweka ambao wanajua CCM inataka nini kwao,”Alisema Polepole.

Sambamba na hilo alisema kuwa CCM imekuwa ikilaumiwa kwa utekelezaji duni wa miradi kutopeleka maendeleo kwa wananchi lakini jambo hilo lipo mikononi mwa wakuu wa idara katika halmashauri nchini hivyo amewataka kutimiza wajibu wao katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.

Akizungumzia uchaguzi mkuu unaokuja kiongozi huyo amewataka viongozi na wanachama wa CCM mkoani Kigoma kuungana na kuwa kitu kimoja katika kusimamia kampeni za chama hicho ili kiweze kupata ushindi kwani makundi ndani ya CCM yamefanya chama hicho kupoteza jimbo la Kigoma mjini kila wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles