25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

CCM KUTOMJADILI MANJI

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, kimesema hakitamjadili Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, Yusuph Manji, hadi kesi yake itakapomalizika mahakamani.

Msimamo huo umekuja baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba chama hicho kimepanga kumjadili Manji kuhusiana na tuhuma zinazomkabili ambapo taarifa hizo zilieleza kuwa diwani huyo atajadiliwa vikaoni ili afukuzwe uanachama kwa kuwa chama hicho hakitaki wanachama wenye tuhuma na wanaovunja amri za nchi.

“Kikao cha kamati tendaji ya chama kitaitishwa mapema mwezi huu kutekeleza maazimio ya vikao vilivyokwishafanyika kuanzia tawi hadi kata ambavyo vilikuwa na agenda ya kumjadili Manji kuhusu tuhuma zake,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema, alisema hawawezi kuingilia suala ambalo bado liko kwenye vyombo vya sheria.

“Wakati utakapofika na ikaonekana ipo sababu baada ya vyombo husika vya kisheria kama mahakama kumtia hatiani, kama chama tutakaa tuangalie katiba yetu inatuelekeza vipi na hapo ndipo tutachukua hatua,” alisema Sikunjema.

Wiki iliyopita Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidaiwa kutumia dawa za kulevya, hata hivyo alikana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles