25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

CCBRT yatoa vifaa kujikinga na Corona vituo vya afya 33 Dar

Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MKURUGENZI  Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi, amekabidhi vifaa maalumu vya kujikinga uso (Face Shields) 150 kwa hospitali na vituo vya afya 22 katika Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam ili kitumiwa na wahudumu wa afya kujikinga  na Covid-19.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msangi alisema lengo la CCBRT ni kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wengine katika kuwakinga wahudumu wa afya na janga la Corona. 

“Tumekusudia vifaa hivi vitumike katika vitengo vya afya ya uzazi katika hospitali hizo ili kuwakinga wahudumu wa afya ambao kila siku wamekuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto”,alisema.

Msangi alisema vifaa hivo vitasaidia kuwaweka salama watoa huduma wakati wakiwahudumia wagonjwa hasa wale wenye dalili za Corona.

“Ni jukumu la watu wote kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali katika mapambano hayo ya Corona, hivyo natoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuweka mkono katika hili bila kujali ukubwa na udogo wa msaada unaotolewa mimi nafikiri msaada ni msaada tu,”alisisitiza Msangi.

Kwa takribani kipindi cha miaka 10, CCBRT kwa kushirikiana na Timu ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam (RHMT) na Timu za Afya za Manispaa (CHMTs), wamekuwa wakiendesha mradi wa kujenga uwezo wa watumishi wa afya eneo la afya ya uzazi katika hospitali, vituo vya afya na zahanati 22 katika manispaa zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam. 

Kwa sasa mradi huu pia unafanya kazi na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mloganzila hasa kwenye upande wa rufaa za wagonjwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles