22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

CBA yaungana na Serikali mapambano dhidi ya corona

Na ASHA BANI

BENKI ya Biashara Afrika (CBA) Tanzania Limited imeungana na Serikali katika kuhakikisha inapambana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Katika hilo, CBA imetoa msaada wa matanki ya kuwekea maji yenye thamani ya Sh milioni 10 kwa hospitali kubwa nne za jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuunga mkono mapambano ya ugonjwa huo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa Hospitali ya Mwananyamala, Amana, Lugalo na Sinza, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CBA, Gift Shoko alisema hiyo ni hatua ya awali ya kuunga mkono Serikali na jamii.

“Lengo la kufanya hivi ni kuonyesha jinsi gani benki inaendelea kujali jamii na watu wake, inajali wateja na pia kushirikiana na Serikali kwani pasipo kujilinda ugonjwa huu ni hatari pia,” alisema Shoko.

Aliongeza kuwa mchango huo ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na CBA katika kuunga mkono jitihada za Serikali kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa Covid–19 nchini.

“CBA imeweka nia thabiti ya kusaidia hospitali kwa kugawa vifaa vinavyohitajika kutakasia mikono ili watu waweze kunawa mikono kama njia muhimu ya kuzuia maambukizi.

“Mara baada ya kuona ongezeko la mahitaji ya kunawa mikono, CBA ilianza mchakato wa kuandaa matenki ya kuhifadhia maji ili kuwezesha watu kunawa mikono wanapokuwa hospitalini, maeneo ambayo ni muhimu kwa afya ya wakazi wa Dar es Salaam.

“Kama tunavyojua, virusi vya corona pia huenea kwa kugusa maeneo yaliyo na maambukizi, hivyo tumehakikisha kuwa matenki hayo yana pedali za miguu ili kuwakinga zaidi watumiaji wa matenki hayo,” alisema Shoko.

Alisema CBA inatoa elimu kupitia barua-pepe, ujumbe mfupi wa simu, mabango katika maeneo mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii (Facebook na Twitter) ili kutoa taarifa sahihi kuhusu Covid-19 na jinsi ya kulinda, kuzuia maambukizi na kuchukua hatua mbalimbali.

“CBA imeweka msisitizo mkubwa kwenye usalama wa wafanyakazi na wateja wetu kwa kuweka vitakasa mikono katika njia zote za kuingia benki na katika vyumba vyote kwa matumizi ya wateja na wafanyakazi,” alisema Shoko. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles