24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

CBA, Vodacom wafunga kampeni miaka mitano ya M-Pawa

Mwandishi wetu – Dar es Salaam

Promosheni ya kusherehekea maadhimisho ya miaka mitano ya M- Pawa iliyokuwa ikiendeshwa na benki ya

CBA na kampuni ya Vodacom, imefika tamati leo Alhamisi Julai 18, ambapo mshindi wa kwanza Andrisa Mathias, (27) kutoka Geita amezawadia sh milioni 15 na wengine 339 wakiondoka na mara 2 ya akiba yao, Simu kali na muda wa maongezi.

Droo hiyo kubwa imeendeshwa kwenye makao makuu ya benki ya CBA yaliyopo Posta jijini Dar es salaam, mbele ya Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya bahati nasibu, Humudi Abdal Hussein, Wawakilishi kutoka benki ya CBA Yessie Yassin na Maria Marbella, mwakilishi kutoka Kampuni ya Vodacom Alice Lushiku, watangazaji maarufu Dokii na Mpoki ambao pia ni mabalozi wa huduma ya M-Pawa na waandishi mbalimbali wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi Mkuu wa M-Pawa benki hiyo ya CBA, Gloria Njiu, amesema huduma ya M-Pawa inalenga kuwaendeleza na kuwawezesha watanzania wengi hususan wasiofikiwa na huduma za kibenki pamoja na wajasiriamali wadogo.

“Benki ya CBA inajivunia safari hii ya miaka mitano ya mafanikio ya huduma hii na inawapongeza wateja wote walioshinda hususani Andrisa,ambaye ni mshindi mkubwa wa promosheni hii.

Akiongea kwa njia ya simu mshindi huyo wa milioni 15, ameonesha kufurahishwa na ushindi huo ambapo ametoa shukrani zake kwa benki ya CBA na kampuni ya Vodacom, kwa kuwawezesha wateja wake kupitia kampeni hiyo na kuahidi kuendelea kuwa mtumiaji mzuri wa huduma hiyo kutokana na faida zake.

Naye mwakilishi kutoka kampuni ya Vodacom, Alice Lushiku, amewapongeza washindi wote na kuwahimiza kuendelea kuhifadhi akiba zao na kurudisha mikopo yao mapema ambapo amewataka watu wote ambao sio wateja wa M-Pawa kujiunga na huduma hiyo ili iweze kuwajumuisha katika ulimwengu wa kifedha hususani kwa watu ambao hawafikiwi na huduma za kibenki kwa urahisi.

Andrisa atakabidhiwa zawadi yake Jumamosi Julai 20, katika hafla fupi itakayofanyika Lugalo jijini Dar es Salaam, kuadhimisha miaka mitano ya huduma hiyo nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles