24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Cardi B, Offset wafanya kufuru kwa mtoto wao

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Offset na mke wake Cardi B, wameonesha jeuri ya fedha kwa kutumia dola 100,000 kumnunuria mtoto wao Kulture cheni ya shingoni.

Wawili hao waliamua kununua cheni hiyo kwa ajili ya kumfanya asherehekee siku yake ya kuzaliwa, ambapo anatimiza mwaka mmoja tangu azaliwe.

Dola 100,000 za Kimarekani ni zaidi ya milioni 229 za Kitanzania, hivyo nyota hao wa muziki wa hip hop wameamua kuziteketeza fedha hizo kwa mtoto wao.

“Najivunia kuwa mzazi, acha nimpende mwanangu, huu ni mwaka wake wa kwanza kufanyiwa sherehe ya kuzaliwa kwake ikiwa anatimiza mwaka mmoja,” aliandika Cardi B.

Hata hivyo kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, wawili hao wametenga bajeti ya dola 400,000 kwa ajili ya sherehe hiyo, ambazo ni zaidi ya milioni 917.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles