CARDI B AUANIKA UJAUZITO WAKE

0
868

LOS ANGELES, Marekani


STAA wa muziki wa hip hop, Cardi B, amethibitisha taarifa zilizokuwa zimeenea katika mitandao ya kijamii, zikimtaja kuwa na ujauzito.

Kwa miezi mingi sasa, rapa huyo amekuwa akikanusha kila alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya ujauzito wake.

Cardi B mwenye umri wa miaka 25, juzi hakuwa na cha kuficha tena kwani tumbo lake lilionekana wazi wakati alipohudhuria tamasha la vichekesho la ‘Saturday Night Live’.

Alipanda jukwaani kutumbuiza akiwa ametinga gauni lake la rangi nyeupe ambalo lilionekana kumbana, kiasi cha kukifanya ‘kibendi’ chake kionekane.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ambao ni maarufu kwa habari za mastaa, Cardi B, anayetoka kimapenzi na rapa mwenzake, Offset, atajifungua Juni, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here