28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Cardi B apambana na mwanawe kuita mama 

Cardi B apambana na mwanawe kuita mama

MSHINDI wa tuzo za Grammy kwa albamu bora ya muziki wa hip hop kwa wanawake, Cardi B, ameendelea kupambana na mtoto wake, Kulture, ili kuhakikisha anaanza kutamka neno mama badala ya baba.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 26, alitumia ukurasa wake wa Instagram akiposti video yake akiwa na mtoto huyo mwenye umri wa miezi sita, akimlazimisha kusema neno mama.

Siku za hivi karibuni mrembo huyo aliwahi kusema, atajisikia vibaya endapo atakuja kumsikia mtoto wake akianza kusema neno baba badala ya mama kama anavyotarajia.

Cardi B alisema amekuwa akitumia muda mwingi kuwa na mtoto wake, tofauti na ilivyo kwa baba wa mtoto huyo, Offset, hivyo atashangaa mtoto huyo kuona anaanza kuita baba badala ya mama.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,312FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles