26.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 15, 2021

CARDI B AMUOMBA RADHI BRUNO MARS

CALIFORNIA, MAREKANI

RAPA Belcalis Almanzar, maarufu kwa jina la Cardi B, amemuomba radhi msanii mwenzake Bruno Mars kwa kusitisha kuungana naye kwenye ziara yake ya muziki ijulikanayo kwa jina la 24K Magic Tour.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo aliweka wazi sababu ya kushindwa kuungana kwenye ziara hiyo kuwa umri wa mwanaye ni mdogo.

“Nienza kwa kumuomba radhi Bruno Mars kuwa sitoweza kuungana naye kwenye ziara yake ya 24K Magic Tour ambayo inatarajia kuanza Septemba, nitashindwa kuungana naye kwa kuwa bado mwanangu ni mchanga sana, hivyo daktari wangu amenishauri nisifanye ziara yoyote ya muziki,” aliandika.

Hii ni wiki ya pili tangu mrembo huyo afanikiwe kupata mtoto wake wa kwanza na rapa mwenzake Offset kutoka kundi la Migos

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
161,753FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles