23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Cardi B ajiachia bila pete ya ndoa

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya Cardi B kuthibitisha kuachana na baba wa mtoto wake, Offset, mrembo huyo ameanzakuonekana mitaani bila pete ya ndoa.

Kitendo hicho kinaonesha wazi kuwa wawili hao wameachana tofauti na watu wanavyodhani kuwa ni sehemu ya kiki katika kazi zao za muziki.

Jumanne wiki iliyopita mrembo huyo alitumia ukurasa wa Instagram na kuweka wazi kuwa, hawapo kwenye ndoa tena kwa kuwa kila mmoja hakuzaliwa kwenye familia zenye upendo ndani yake.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 26, mwishoni mwa wiki iliyopita alionekana kwenye ‘red carpet’ ya Jingle Ball huko jijini New York bila ya pete ya ndoa ambayo alivishwa na rapa huyo mara baada ya kufunga ndoa ya siri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles