27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Cannon ataja chanzo bifu na Eminem

NEW YORK, MAREKANI

MUME wa zamani wa Mariah Carey, Nick Cannon, ameweka wazi chanzo cha ugomvi wake na rapa Eminem ni mke wake.

Cannon aliongea maneno hayo wakati wa mahojiano na kipindi cha Daytime Talk Show, alisema hakuwa na lengo la kutaka kuingia kwenye mgogoro na Eminem lakini aliyekuwa mke wake Mariah ndiyo chanzo.

“Mariah na Eminem walikuwa na bifu lao wenyewe, hivyo sikuweza kuwa mnyonge hasa pale rapa huyo alipomzungumzia mke wangu kwenye wimbo wake wa Bagpipes from Baghdad, nikaona na mimi nionyeshe uwanaume wangu.

“Eminem hakuwa na shida na mimi, lakini nilinunua kesi, mwisho wa siku sisi ni wanaume, nikaona nikae chini kujaribu kuyamaliza ila haikuwa kazi rahisi,” alisema Cannon.

Bifu hilo lilianza mwaka 2009, kabla ya Cannon na Mariah kuachana 2014 huku tayari wakiwa na watoto wawili mapacha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles