24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

CAMPBELL: TANZANIA IKIWEKEZA KWA VIJANA ITATOKA

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell, amesema njia pekee ya kulikwamua soka la Tanzania ni kuwekeza katika kuibua na kuendeleza soka la vijana.

Campbell alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza na watoto wa kituo cha kuendeleza vipaji vya soka cha  Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Beki huyo alisema kwa kuwekeza katika soka la vijana kutalifanya soka la Tanzania kuanzia katika ngazi ya klabu hadi timu za taifa kupiga hatua ya kimaendeleo.

“Soka linahitaji uwekezaji mkubwa hasa eneo la kusaka vipaji ambavyo vimetapakaa dunia kote, viongozi wanatakiwa kuhakikisha wanasaka vipaji vya vijana na kuvilea katika misingi bora ya soka kwa ajili ya maendeleo ya Taifa,” alisema.

Kwa upande wake, mwanzilishi wa kituo cha kuibua na kuendeleza vipaji cha Gymkhana, Juma Maswanya, alisema kitendo cha mchezaji huyo kuwatembelea kimewapa hamasa kubwa watoto hao pamoja na kujifunza mambo muhimu wanayopaswa kufuata ili wafanikiwe.

“Tumepokea kwa furaha ujio wa Campbell hapa nchini, pia kuja kwake katika kituo chetu kuangalia namna tunavyoandaa vijana kwa ajili ya kuinua soka la Tanzania.

“Hii fursa adhimu kwa watoto, kwani sasa watapata uzoefu wa mchezaji huyo baada ya kukutana naye, watoto hawa sasa watamfanya Campbell kama mfano wao katika kujifunza soka,” alisema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles