23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Camel Oil: Tulifuata sheria kuuza kituo cha mafuta Manzese

Camel OilNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MENEJA wa Kampuni ya Camel Oil, Mahfoudh Ally, amesema kiwanja namba 130, Block A kilichopo Manzese Dar es Salaam, ambacho kinabishaniwa kiliuzwa kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Ally alisema hayo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo alisema taarifa mbalimbali zinazosambazwa kuhusu uwanja huo ni za kupotosha.

“Kampuni ilifuata taratibu, baada ya mmiliki wa awali, Mzee Mohammed Fakhi, kushindwa kulipa deni la Sh bilioni 1.4, uamuzi wa kuuza ulikuwa wa mwisho baada ya jitihada za muda mrefu kugonga mwamba.

“Mwaka 2010, kampuni ilifanya biashara kwa muda mrefu na Mzee Mohammed wa Manzese Filling Station kuhusiana na kuuza mafuta kwa mkopo kwa makubaliano kwamba, Camel ilipwe kila mwezi,” alisema Ally.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema kampuni yake iliendelea kukipa kituo hicho mafuta lakini mmiliki aliendelea kulimbikiza madeni hadi kufikia Sh bilioni 1.6 na mwaka 2012, aliacha kununua mafuta kwenye kampuni hiyo bila kutoa taarifa.

“Mohammed alikubali kuweka dhamana kiwanja namba 130 Kitalu A Manzese, chenye thamani ya Sh milioni 850 na kiwanja namba 861 na namba 862 cha Msasani vyenye thamani ya Sh milioni 300.

“Baada ya jitihada zote kushindikana, tulimtafuta dalali kwa ajili ya kuuza kiwanja hicho cha Manzese ili kufidia deni, Kampuni ya Udalali ya Bilo Star Debt Collection, ilipewa kazi ya mnada uliofanyika Julai 9 mwaka huu na Kampuni ya State Oil ilipata kiwanja hicho kwa kukinunua kwa Sh bilioni moja.

Hata hivyo, alisema suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria hivyo wanatarajia litamalizika huko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles