26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

CAG avilalamikia vyama vya siasa

NA ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, amesema vyama vya siasa vilishindwa kuwakilisha kwa wakati hesabu za mwaka 2013/2014 kama ilivyopangwa kisheria.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipozindua ripoti ya tatu kwa wananchi iliyolenga jinsi ya kutatua matatizo yanayowakabili ikiwa ni wiki moja baada ya Msajili Msaidizi Kitengo cha Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Piencia Kiure, kuvitaka vyama vya siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kupeleka ripoti ya hesabu za gharama zao.

Kiure alitaja vyama hivyo vilivyowasilisha ripoti ya gharama za uchaguzi kuwa ni Chama cha ACT Wazalendo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Katika hatua nyingine, CAG alisema watumishi wa mashirika ya umma wametakiwa kuwa na matumizi mazuri ya fedha zilizotengwa katika bajeti mbalimbali  kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Alisema kwa mwaka wa fedha uliopita kulionekana kuwa na udhaifu mbalimbali yaliyosababishwa na baadhi ya watumishi hao ikiwemo mwaka wa fedha wa 2013/2014.

“Kulionekana kuwa na udhaifu ikiwamo Serikali kulipa jumla ya shilingi milioni 543.79 ambayo ni malipo ya posho na kodi za nyumba kwa watumishi waliostaafu na wasio na mikataba waliopo ubalozini, hivyo hali hiyo isijirudie tena katika mwaka huu wa fedha,” alisema Profesa Assad.

Kuhusu ripoti aliyoizindua, alisema lengo ni kushirikiana na wadau katika kutoa elimu kwa wananchi ili kushiriki katika dhana nzima ya uwajibikaji na usawa.

Alisema ripoti hiyo imelenga kutoa fursa kwa wananchi kwa kutoa maoni yao kuhusiana na utendaji kazi wa Ofisi ya CAG na kupata mrejesho wa ripoti zilizopita ili kuibua changamoto, matatizo na kuyadhibiti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles