24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

CAF yatangaza gharama za kushudia mechi za AFCON

Lulu Ringo, Dar es salaam

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali ya Kombe la Mataifa Africa (AFCON) inayotarajia kuanza mwezi Juni nchini Misri.

Akizungumza na Mtanzania Digital, leo Mei 17, Ofisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema tiketi hizo zitauzwa kwa dola za kimarekani huku wahitaji wakitakiwa kuwasilisha fedha hizo katika shirikisho hilo ili liweze kuwasiliana na CAF kwa upatikani wa tiketi hizo.

“CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  tiketi za daraja la kwanza zikiwa ni dola za kimarekani 29, tiketi za daraja la pili dola za kimarekani 18 na tiketi za daraja la tatu dola za kimarekani sita.

“Kwa yeyote anaehitaji tiketi hizo awasiliane na TFF na atapaswa kulipia kwa dola za kimarekani  kulingana na daraja husika analotaka hivyo shirikisho litawasiliana na CAF na kuwajuza idadi ya tiketi zinazohitajika, amesema Ndimbo.

Katika hatua hiyo ya makundi Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria

Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja la kwanza itakuwa ni dola za kimarekani 35, daraja la  pili dola za kimarekani 24 na daraja la tatu dola za kimarekani 12

Hatua ya nusu fainali daraja la kwanza dola za kimarekani 59, daraja la pili dola za kimarekani 29 na daraja la tatu dola za kimarekani 18.

Wakati mchezo wa mshindi wa tatu itakua dola za kimarekani 35 daraja la kwanza, dola za kimarekani 24 kwa daraja la pili na dola za kimarekani 12 kwa daraja la tatu.

Mchezo wa fainali daraja la kwanza dola za kimarekani 106, daraja la pili dola za kimarekani 44 na daraja la 3 dola za kimarekani 24.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles